Sikio (Ear) limegawika katika sehemu tatu kuu. Sehemu ya nje ya sikio, sehemu ya kati ya sikio na sehemu ya ndani ya sikio.
Kuna aina mbili ya matatizo ya masikio nayo ni:
i. Otitis media : ambayo hutokea katika sehemu ya kati ya sikio na mara nyingi huwatokea watoto wachanga na watoto wadogo.
ii. Otitis externa: ambayo hutokea katika sehemu ya ndani ya sikio na mara nyingi huwatokea waogeleaji, na hutokea zaidi wakati wa baridi.
Ishara za Matatizo ya masikio kwa Otitis media:
i. Kuumwa na kuchomwa kwa sikio
ii. Kutokwa na uchafu ndani ya sikio
iii. Kutosikia kwa ghafla
iv. Homa
Sababu za Otitis media:
Sababu kubwa ya maradhi hayo ni kuziba kwa bomba la sikio(Eustachiantube), kutokana na baridi, allergy pamoja na kuingia takataka. Hii inababisha maji maji ya sikio kujaa maji hayo nayo husababisha uvimbaji wa (ear drum) sikio.
Sababu za Otitis externa:
Hii husababishwa na baketeria au fungi, maji maji yanayoingia ndani ya sikio ndio sababu kuu ya kufanya bakteria na fungi kuzaana pia Skin allegies husababisha maradhi hayo.
Na sababu nyengine ni ulaji mbovu wa chakula pamoja na upungufu wa usafi wa mwili.
DAWA ZA KUJITIBU MARADHI YA MASIKIO:
i. Nyunyiza juisi ya Kitunguu saumu katika sikio linalouma
ii.v Nenda Hospitali ukapigwe bomba ili maji na uchafu upate kutoka
iii. Pasha moto mafuta ya Zaituni (Olive oil) na yasubiri yapowe na ujitie drops mbili hadi 3
iv. Na usafishe masikio yako kila baada ya kutoka kukoga.
KUTOKWA NA USAHA SIKIONI:
Ikiwa utaweka kitu kama ujiti wa kiberiti au mfano wake sikioni, unaweza kusababisha jeraha kwenye sikio na damu kuanza kutoka. Baadae usaha unaweza kutungwa sehemu ya jeraha na kutoka kidogokidogo. Lakini pia mashambulizi ya bacteria sikioni yanaweza kusababisha kutokwa na usaha.
TIBA ZA MAUMIVU YA MASIKIO NA KUTOKWA NA USAHA:
Kanuni ya kwanza:
Chukua maji masafi ujazo wa kijiko kimoja cha chai halafu uchukue chumvi kidogo kiasi cha vidole viwili uchanganye ndani ya maji hayo kisha hayo maji uchanganye na asali kijiko kimoja kidogo cha chai. Weka tone moja ya dawa hii ndani ya sikio lenye kuuma au kutokwa na usaha kutwa mara tatu.
Kanuni ya pili:
Dondoshea tone moja ya mafuta ya kitunguu saumu ndani ya sikio ambalo linauma au kutokwa na usaha kutwa mara tatu..
Kanuni ya tatu:
Chukua mafuta ya habat soda na ufanye kama kanuni ya pili.
Kanuni ya nne:
Ikiwa maradhi ya sikio ni kwa ajili ya bacteria, kunywa antibayotiki asilia kama vile juisi ya Aloe vera, kitunguu saumu, n.k. E.
HABARI ZA MICHEZO, SIASA, UCHUMI, ELIMU NA MATANGAZO YA BIASHARA TUNAPATIKANA KWA NAMBA ZIFUATAZO +255785312020 KWA SIMU ZA KAWAIDA NA Whatsapp
Friday, March 18, 2016
KILIMO RAHISI CHA UYOGA KWA WAKULIMA WADOGO WADOGO.
Habarini ndugu zangu wakulima na wadau wote wa Kilimo. Nilikwisha wahi andika juu ya Kilimo bora cha Uyoga, na kueleza kwa kina ni jinsi gani mkulima anaweza kunufaika na kilimo hiki. Lakini basi leo ningependa nifundishe juu ya Kilimo rahisi kabisa cha zao hili la Uyoga ambapo hata mkulima mdogo kabisa huko kijijini anaweza kumudu katika kilimo hiki.
Namna ya kuotesha Uyoga.
Kabla ya kuzalisha uyoga inabidi kuwa na chumba chenye paa ambalo litazuia jua, mvua na vumbi. Chumba hiki kinatakiwa kiwe na sakafu inayohifadhi unyevunyevu pamoja na sehemu ya giza ambayo ni muhimu kwa kuotesha utando wa Uyoga. Mkulima wa kawaida anaweza kutumia kasha kama sehemu ya giza.
Hatua muhimu katika kuotesha Uyoga baada ya kupata mbegu ni kama ifuatavyo:
. Kusanya masalia ya mazao kama vile mabua, majani ya mpunga, ngano, Pumba za mpunga au mahindi, masalia ya miwa baada ya kukamua n.k
Vitu hivi hutumika kama mali ghafi kwa kuoteshea Uyoga.
. Mabua, Majani ya Mpunga au Migomba yakatwe kwa urefu usiozidi sentimeta 6, au urefu wa vidole kwa kutumia panga au kisu.
. Loweka mali ghafi kwenye maji ya kawaida kwa muda wa siku nzima ( saa 24).
. Kisha yachemshwe kwa muda wa saa 2 ili kuua vijidudu pamoja na vimelea vilivyomo.
. Ipua na umwage maji yote halafu tandaza kwenye kichanja kisafi ili yapoe bila kuchafuliwa na vumbi au vijidudu.
. Kisha jaza mali ghafi hii katika mifuko ya nailoni tayari kwa kupanda mbegu.
Namna ya kupanda.
Kuna aina mbili za upandaji;
AINA YA KWANZA
Chukua mfuko wa nailoni, weka tabaka ya mali ghafi ya kuoteshea kiasi katika mfuko halafu tawanya mbegu juu yake.
Baada ya kuweka mbegu, weka tena tabaka nyingine ya kuoteshea na kuweka mbegu juu yake.
Endelea kuongeza tabaka kwa namna hii mpaka ifikie ujazo wa robo tatu ya mfuko.
NB: Tabaka la mwisho la juu lazima liwe la vioteshea.
AINA YA PILI
Changanya mali ghafi ya kuoteshea ( baada ya kuchemsha na kupoa) na mbegu ya uyoga katika uwiano wa 1:25 ( mbegu : mali ghafi ya kuoteshea).
Kwa uyoga aina ya Mamama ( Pleurotus spp), kisha mchanganyiko huu ujazwe katika mifuko ya nailoni. Mifuko hii iwe ya ukubwa wa sm 20 kwa sm 40 ambamo unaweza kujaza kilo 1-1.5 ya mali ghafi ya kutosha.
Katika njia zote mbili, funga mifuko na toboa matundu kwenye mifuko yenye kipenyo cha sm 6 hadi 10 kwa kila mfuko.
Zingatia:
(i) Matundu yawe mengi ili kuingiza hewa ya kutosha ndani ya mifuko.
Uyoga ni Kiumbe hai, hivyo unahitaji kupumua.
(ii) Ukishanunua mbegu, kama hupandi kwa muda huo, hifadhi kwenye jokofu. Kama huna jokofu, nunua mbegu baada ya kuandaa kila kitu. Mbegu za uyoga zinaweza kuota vizuri hata zikikaa nje ya jokofu kwa siku mbili.
(iii) Waweza kutumia chupa moja yenye ujazo wa mililita 300 kwenye kilo 15 za mali ghafi ya kupteshea. Hakikisha unamaliza mbegu yote kwenye chupa kwani ikibaki itapata maambukizo ya vimelea.
(iv) Hakikisha unaponunua mbegu iwe ni nyeupe. Mbegu ambayo siyo nyeupe ni dalili za maambukizo ya vimelea. Vingine na hivyo haifai kupandwa.
Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na Marcodenis E. Misungwi, Agriculture Extension Officer at Mbozi District Council.
MATUNZO YA ZAO LA UYOGA.
Weka mifuko kwenye chumba cha giza. Kwa mkulima wa kawaida waweza kutumia kasha lisilopitisha mwanga kama chumba cha giza.
Acha mifuko humo kwa muda wa siku 14-21 bila kufunua ili ukungu mweupe uweze kutanda vizuri.
Utando wa uyoga ukishatanda vizuri kwenye mali ghafi ya kuoteshea, hamishia kwenye chumba cha mwanga na hewa ya kutosha kisichopigwa jua.
Katika chumba chenye mwanga. Mifuko inaweza kuwekwa kwenye meza, chanja ya waya au miti. Mifuko pia inaweza kuning'inizwa kwenye kamba.
NB: Unaweza kunyunyizia maji juu ya mifuko yaliyochemshwa na kupoa, mara tatu au zaidi kwa siku.
Tahadhari:
Usizidishe maji kwani maji yakiwa mengi sana yanaweza kuozesha uyoga.
Aina nyingi za uyoga huanza kutoa vichwa siku 2-3 baada ya kuwekwa kwenye mwanga.
UVUNAJI WA UYOGA.
Uyoga huwa tayari kuvunwa siku tatu baada ya vichwa kuonekana.
Uyoga uvunwe kwa mkono kwa kushika katikati ya shina la uyoga, kisha zungusha hadi uyoga ung'oke.
Usiondoe kichwa peke yake katika kuvuna uyoga kwa kubakiza shina huzuia uyoga mwingine kutokea.

Namna Unavyoweza Kuondoa Mawazo Hasi Katika Maisha Yako.
Mwanadamu ni kiumbe ambaye amepewa uwezo mkubwa sana wa kufikiri. Na katika uwezo huo huwa mara nyingi anakuwa ana mawazo chanya na mawazo hasi. Mimi na wewe kwa namna moja au nyingine huwa ni watu wa kutumia mawazo haya, yawe chanya au hasi lakini tunakuwa nayo.
Kila siku tunavyoishi huwa tunakuwa na mawazo mengi sana kwani akili ya mwanadamu huwaza kila dakika. Hebu fikiria sasa hivi na jaribu kuandika mawazo yako ambayo unafikiria kwa takribani kila siku. Mangapi kati ya mawazo hayo huwa ni hasi? Naweza kusema kwamba asilimia kubwa ya watu wengi, mawazo yao ni hasi. Naamini utaniunga mkono katika hili.
Je, unajua kwamba mawazo yetu yana nguvu kubwa sana ya ajabu na pia yana uwezo kwa asilimia kubwa sana kubadili maisha yetu. Akili inaweza ikawa ni kitu kigumu sana kukimiliki na kukitawala kama usipokuwa makini. Lakini unapoongeza umakini katika kuitumia akili yako, itakusaidia kufanikisha mipango yako mingi iliyokwama.
Siku zote ukitaka kuwa mchezaji mzuri ni lazima ufanye mazoezi sana. Hivyo basi hata ukitaka ubongo wako kufikiri chanya ni lazima uufanyishe ubongo wako mazoezi mengi sana ya kutosha. Hiyo itasaidia ubongo wako kufikiri kutoka hasi na kuanza kufikiri chanya.
Kwanini ni muhimu sana kuondoa mawazo hasi? Hiyo yote ni kwa sababu mawazo hasi ni kizuizi kikubwa cha kufikia mafanikio yako. Kama ukitaka kuacha kufikiria mawazo hasi kuna njia ambazo unaweza kuzitumia na ukaweza kufikia malengo yako.
Kwanza, soma vitu vya kukufanikisha.
Dunia ya leo ina kelele nyingi sana ambazo ni hasi na hazina maana wala msaada sana kwako. Ili uweze kutoka huko ni muhimu kwako kujilisha au kusoma vitu vya kukufanikisha. Hapa unaweza ukasoma vitabu, majarida ya mafanikio au hata ukahudhuria semina.
Usikubali kukaa kienyeji enyeji, poteza fedha zako kwenye kununua au kusoma vitabu mitandaoni ambavyo vinaweza kukusaidia kukuongeza uwezo wako wa kufikiri chanya. Kwa kujijengea mawazo chanya itakupelekea wewe mwenyewe kufikia ndoto zako.
Pili, fanya tahajudi(Sala).
Wakati mwingine mawazo hasi yanakuwa sio rahisi sana kuondoka mpaka ufanye tahajudi au sala. Hili ni tendo ambalo unaweza ukawa unalifanya kila siku. ‘Kumediteti’ hakuhitaji nguvu kubwa sana, inaweza ikawa rahisi sana na ukafanikiwa kuondoa mawazo hasi.
Unapoanza kutaka kufanya tahajudi au ‘meditation’ funga macho yako, wakati huo huo unavuta pumzi taratibu huku ukiwa umetulia kimya ukitafakari hali unayotaka ikutokee. Unapofanya hivi kwa muda utajikuta unapata majibu na kufanikisha malengio kwa sababu unachukua muda kuuongoza ubongo wako.
Tatu, andika mawazo mazuri.
Baada ya kuhisi kuwa una mawazo chanya yanaanza kuleta mwamko wa mafanikio, unaweza ukawa na kitabu cha kumbukumbu zako( Diary) na ukaamua kuyaingiza yale mawazo unayayona ni mazuri na yanaweza kuleta mabadiliko mara moja
.
Zoezi hili la kuandika mawazo mazuri litakusaidia sana kupunguza mawazo hasi katika akili yako na kwa kuanzia hapo utaupa uwezo ubongo wako kuwaza mawazo chanya na yenye mafanikio kwa upande wako.
Nne, usikate tamaa.
Hata inapotokea unaona mawazo yako hasi kama hayatoki na bado yapo, jifunze kutokukata tamaa mapema. Amini mawazo yako hayo yataanza kutoka polepole. Kitu kikubwa uwe una nia ya kuamini kwamba ni lazima utakuwa una mawazo chanya muda sio mrefu.
Ni matumaini yangu ya kwamba utatumia njia hizo katika kukusaidia kukupa mawazo chanya yenye manufaa kwako na kitaifa pia. Pia usisahau kumwomba Mungu akusaidie.

AINA ZA UPUNGUFU WA DAMU MWILINI (ANAEMIA)
Leo tuangalie tatizo la upungufu wa damu mwilini. Anaemia ni jina la jumla linalotumiwa kubainisha aina mbalimbali za upungufu wa damu mwilini.
Kiwango cha kawaida cha chembe nyekundu za damu (Haemoglobin-Hb) katika mwili wa binadamu ni kati ya gramu 12 mpaka 14 kwa kila mililita ya damu na zikiwa pungufu ya hapo mtu huyo anakuwa na tatizo la upungufu wa damu.
Upungufu wa damu mwilini hutokea iwapo mkusanyiko wa pamoja wa chembe nyekundu za damu zinapopungua kupita kiwango cha kawaida kinachotakiwa kwenye mwili wa binadamu.
Tatizo hili linaweza kumpata mtu yeyote ingawa visababishi vinaweza kutofautiana.
Licha ya utofauti huo mara nyingi tatizo hili husababishwa na mambo makuu matatu ambayo ni kupoteza damu mfano wakati wa hedhi kwa wanawake hasa wanaotokwa na damu nyingi au kuvuja damu kunakosababishwa na vidonda vya tumbo.
Sababu nyingine ni uzalishwaji duni wa chembe nyekundu za damu unaosababishwa na upungufu wa vitamini au lishe duni pamoja na magonjwa sugu. Pia magonjwa ya kurithi.
Iwapo mtu atapungukiwa kiasi cha madini, ulaji wa madini ya chuma katika mlo wa kawaida wa mtu hauwezi kufidia kiwango cha madini kilichopotea na kiasi hicho kinachokuwa kimebaki hutumika mara moja.
Aina za upungufu wa damu mwilini
Zipo aina mbalimbali za upungufu wa damu ikiwemo Haemolytic Anaemia. Hali hii ya upungufu wa damu, chembe nyekundu za damu huharibiwa haraka kuliko mwili unavyoweza kuzalisha chembe nyingine.
Upungufu huu husababishwa na mambo mengi ikiwemo kansa aina ya Lymphoma au utumiaji wa baadhi ya dawa ambazo huweza kuangamiza chembe nyekundu za damu kwa mfano dawa aina ya Methylodopa inayotibu matatizo ya presha ya kupanda.
Mtu mwenye aina hii ya upungufu wa damu anaweza kupatwa na homa, kutetemeka kwa mwili, maumivu ya tumbo na mgongo na mapigo ya moyo kushuka ghafla.
Pernicious Anaemia. Huu ni upungufu wa damu unaotokana na ukosefu wa kutosha wa asidi aina ya Folic (Folate) katika chakula.
Asidi aina ya Folate hupatikana katika mbogamboga za rangi ya kijani, matunda na nyama.Aplastica Anaemia. Huu ni upungufu wa damu unaotokea wakati chembe nyekundu za damu zinaposhindwa kuzalishwa ipasavyo.
Sickle cell Anaemia. Ni aina nyingine ya upungufu wa damu ambao chembe nyekundu za damu huwa na muundo usio wa kawaida unaozuia na kuathiri mishipa midogo ya damu na hivyo kusababisha kuziba kwa mishipa hiyo ya damu.
Dalili za upungufu wa damu mwilini (anaemia)
Mtu mwenye tatizo la upungufu wa damu mara nyingi huwa amepauka mwili na hujisikia kuchoka, udhaifu na huwa na mwendo kasi wa damu (yaani high pulse rate). Mgonjwa kuhisi kiu, kizunguzungu wakati akisimama, moyo kwenda kasi wakati akitumia nguvu kufanya jambo lolote, kuhema mfululizo na kupumua haraka haraka.
Dalili nyingine ni mapigo ya moyo kwenda kwa kasi, kuhisi uchovu sana au hata kuishiwa kabisa na nguvu. Wakati mwingine mgonjwa anaweza kuhisi maumivu ya kifua pamoja na kuchanganyikiwa anaposhughulikia jambo fulani.
Kuvimba kwa tumbo au sehemu za chini yake, kupoteza nguvu na macho kukosa nuru ya kuona vizuri ni dalili nyingine za mtu mwenye tatizo hili.
Matibabu yake
Matibabu ya upungufu wa damu aina yoyote yanategemea aina ya upungufu wa damu inayomkabili mgonjwa.
Upungufu wa damu hutibiwa mapema kwa kubadili lishe pamoja na kuongeza lishe yenye vitamini C na B12 pamoja na madini ya chuma kutokana na visababishi vya tatizo.
Matibabu ya lishe yanaweza kutumika kwa ushauri wa daktari ingawa yanaweza yasitoshe hadi pale mgonjwa atakapoongezewa damu.
Mara nyingine vidonge na sindano zenye lishe hizo huweza kutumiwa na madaktari hospitalini sambamba na matibabu ya tatizo linalosababisha na iwapo mgonjwa yuko mahututi huweza kuongezewa damu. Ushauri, ukiona dalili hizo, muone daktari haraka
AINA ZA UPUNGUFU WA DAMU MWILINI -2
Katika makala ya wiki iliyopita tuliangazia tatizo la upungufu wa damu mwilini wengine huita Anaemia ambalo ni jina la jumla linalotumiwa kubainisha aina mbalimbali za upungufu wa damu mwilini.
Tukasema kiwango cha kawaida cha chembe nyekundu za damu (Hb) katika mwili wa binadamu ni kati ya gramu 12 mpaka 14 kwa kila milimita ya damu, zikiwa pungufu ya hapo mtu huyo anakuwa na tatizo la upungufu wa damu.
Tulitaja aina za upungufu wa damu kama vile Pernicious Anaemia na Aplastica Anaemia. Sasa endelea…
Sickle Cell Anaemia:
Ni aina nyingine ya upungufu wa damu ambao chembe nyekundu za damu huwa na muundo usio wa kawaida unaozuia na kuathiri mishipa midogo ya damu na hivyo kusababisha kuziba kwa mishipa hiyo ya damu.
DALILI ZA UPUNGUFU WA DAMU
Mtu mwenye tatizo la upungufu wa damu mara nyingi huwa amepauka mwili na viganja na kucha kuwa nyeupe na hujisikia kuchoka, udhaifu na huwa na mwendo kasi wa damu (yaani High Pulse Rate) na macho yake huwa meupe.
Dalili nyingine ni mgonjwa kuhisi kiu, kizunguzungu wakati akisimama, kuwa na mahangaiko ya moyo wakati akitumia nguvu kufanya jambo lolote, kuhema mfululizo na kupumua harakaharaka, mapigo ya moyo kwenda kwa kasi, kuhisi uchovu au hata kuishiwa kabisa na nguvu.
Dalili nyingine ni kusikia maumivu ya kifua pamoja na akili yake kushindwa kufikiri sawasawa, vilevile kuvimba kwa tumbo au sehemu za chini yake, kupoteza nguvu na macho kukosa nuru ya kuona vizuri.
VIPIMO NA MATIBABU
Uchunguzi wa wingi wa damu hufanyika kwa kupima kiasi cha mkusanyiko wa pamoja wa chembe nyekundu za damu kitaalamu huitwa Haemoglobin pamoja na kufanya kipimo kingine cha damu kijulikanacho kama Peripheral Smear.
Vipimo vingine vya maabara ni pamoja na kipimo cha kufahamu uwezo wa kuhifadhi madini ya chuma yaani Total Iron Binding Capacity (TIBC), kiasi cha Feritin katika damu pamoja na kiasi cha Folic Acid.
Aidha, katika mazingira mengine kipimo cha kuchukua sehemu ya supu ya mifupa na kuichunguza maabara yaani (Bone Marrow Biopsy) kinaweza kufanywa, japo si mara kwa mara.
Matibabu ya upungufu wa damu aina yoyote yanategemea aina ya upungufu wa damu unaomkabili mgonjwa.

Licha ya hiyo, matibabu ya lishe yanaweza kutumika kwa ushauri wa daktari ingawa yanaweza yasitoshe hadi pale mgonjwa atakapoongezewa damu.
Mara nyingine vidonge na sindano zenye lishe hizo huweza kutumiwa na madaktari hospitalini sambamba na matibabu ya tatizo linalosababisha, iwapo mgonjwa yuko katika hali ya mahututi huweza kuongezewa damu.
Tatizo la upungufu wa damu ni tatizo la hatari sana endapo mwenye tatizo hilo atachelewa kupata matibabu mapema. Ukiona dalili hizo wahi kumuona daktari.

Breaking news: Wabunge wa CUF wamejiondoa katika Bunge la Tanzania katika kipindi cha 2015-2020
Katika barua ambayo imesainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Ahmed Nassor Mazrui na kusambazwa kwa wanahabari leo Machi 18,2016, Wabunge wote wa Chama cha Wananchi (CUF) wamejiondoa katika Bunge la Tanzania katika kipindi cha 2015-2020 kwa kile kinachotajwa kama kukiukwa kwa sheria za uchaguzi na kuporwa haki katika uchaguzi wa Zanzibar. Chini ni nakala ya barua kwenda kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai.
JUMA JUX AMESEMA HATAKI MASWALI YA JACK NA VANESSA.
Jux ameweka wazi hisia zake hizo baada ya kufanyiwa mahojiano na eNewz ambapo alisema kuwa yeye pia ni mwanamuziki kama ilivyo kwa Vanessa Mdee na kusema kuwa imejengeka kuwa kila interview anayoifanya ni lazima watu wamuulize kuhusu uhusiano wake na Vanessa na kwasasa imeibuka ya kumuuliza juu ya Jack Cliff.
Jux alishawahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na ‘video vixen’ Jack Cliff ambaye anashikiliwa nchini China kwa kukutwa na madawa ya kulevya na kwasasa staa huyo anajihusisha na mahusiano ya kimapenzi na mwanamuziki mwenzake Vanessa Mdee.
Jux anasema kuwa kuna mambo mengi sana ya kuzungumza kwenye interview ambayo yatakuza muziki wake mbali ya kuzungumza mambo ambayo yatakuwa hayasaidii mahusiano yake wala muziki wake.
Share: Facebook Twitter Google+

Thursday, March 17, 2016
TARIFA YA TRA KUHUSU WAFANYA BIASHARA KUFUNGA MADUKA
Mojawapo ya wajibu wa kisheria wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ni kukagua taarifa za wafanyabiashara ili kuhakiki usahihi wa kumbukumbu za biashara.
Katika kutekeleza zoezi hili, TRA imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuwaelimisha wafanyabiashara juu ya umuhimu wa kutunza kumbukumbu za biashara na kusisitiza utumiaji wa mashine za kielektroniki za kodi (EFDs).
Wakati wa kutekeleza jukumu hilo TRA ilibaini wafanyabiashara wengi wanakiuka sheria za kodi kwa kutokutoa risiti, hivyo wamekuwa wanachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.
Vilevile Mamlaka ya Mapato Tanzania imebaini kuwa kuna njama ya baadhi ya wafanyabiashara kuhamasisha wenzao nchi nzima kufunga biashara kwa makusudi endapo tutaendelea na ufuatiliaji na uhakiki wa bidhaa zilizouzwa bila kutolewa risiti na kutekeleza agizo la serikali la kusitisha matumizi ya kodi elekezi kwa bidhaa zinazoingizwa nchini. Njama hizi ni ukiukwaji wa sheria na hazipaswi kuvumiliwa.
Wafanyabiashara na wananchi wote kwa ujumla wanafahamishwa kwamba kutokutoa risiti baada ya kufanya mauzo au kutoa huduma ya kibiashara ni kosa la jinai linalostahili adhabu.
Hivyo wafanyabiashara wanatahadharishwa kutofunga maduka kutokana na sababu zinazotolewa na wafanyabiashara wanaofanya njama hizo.
Endapo TRA itawabaini wafanyabishara wanaokula njama hizi itachukua hatua kali za kisheria dhidi yao ambazo zitapelekea kuzuiwa kufanya biashara moja kwa moja hapa nchini.
TRA inatoa wito kwa wananchi wote kudai risiti kila wanapofanya manunuzi na kutoa taarifa za wafanyabiashara ambao hawatoi risiti. Vilevile wanaombwa kutoa taarifa katika ofisi yoyote ya TRA za kuwafichua wafanyabiashara wanaokula njama za kuhamasisha wenzao nchi nzima kufunga biashara kwa makusudi.

Subscribe to:
Posts (Atom)