Thursday, March 17, 2016

FANYA YAFUATAYO UWE NA AFYA NJEMA

1.Kunywa kiasi cha kutosha cha maji safi na salama baada ya mazoezi au kazi itakayokufanya utoke jasho na epuka unywaji wa vinywaji baridi kama soda. Unywaji wa maji utasaidia mwili kurudisha maji yaliyopotea mwilini. Maji ni muhimu katika ufanyaji kazi wa mifumo mbali mbali ya mwili.

2.Jifunze kufanya mazoezi ya kunyoosha viungo vya mwili unapoamka, hii husaidia kuboresha mzunguko wa damu, mmeng'enyo na kukusaidia kuondoa maumivu ya
viungo.

3.Kamwe usianze siku yako bila kifungua kinywa. Tafiti zinaonyesha kuwa, kifungua kinywa sahihi ni muhimu hususani kwa wale wanaotaka kupungua uzito. Wale wasiopata kifungua kinywa asubuhi wanakua katika hatari ya kuwa na uzito mkubwa. Mlo kamili kwa kifungua kinywa ni kama juisi za matunda, mkate wa ngano isiyokobolewa, maziwa, mayai na maji.

4.Usitumie vyakula vyenye wanga kabla ya saa moja kupita baada ya mazoezi. Hii itaulazimisha mwili wako kuanza kutumia kiasi cha mafuta yaliyohifadhiwa mwilini badala ya kutumia chakula ulichokula. Unaweza kula matunda katika muda huo ila epuka vinywaji kama bia au soda.

5.Tumia vyakula vyenye Vitamini C kwa wingi, miili yetu huitaji angalau kiasi cha 100mg za Vitamini C kwa siku. Njia bora ya kufikia kiwango hiki ni kadiri ya milo mitano kwa siku ya matunda pamoja na mboga mboga zenye Vitamini hii. Mfano wa vyakula vyenye Vitamini C ni Chungwa, zabibu, pera, embe na mboga za majani.

No comments:

Post a Comment