sickle cell ni nini?
huu ni ugonjwa wa kurithi wa kupungukiwa damu, ambapo mgonjwa hua hana damu ya kutosha kwa sababu ya seli zake za mwili sio imara kubeba hewa ya oksijeni kupeleka sehemu mbalimbali za mwili.
kwa hali ya kawaida seli za binadamu hua na umbo la kama yai na linalovutika kiasi kwamba huweza kupita kirahisi kwenye mishipa ya damu na seli hizo huishi siku 120 yaani miezi mitatu kisha hufa kupisha zingine lakini seli za mgonjwa wa sikoseli ni ngumu yaani zipo kama shepu ya mwezi, huishi siku ishirini tu, na huweza kukwama kwenye mishipa ya damu na kuzuia damu kupita na hichi ndio chanzo kikuu cha matatizo.wagonjwa hawa husumbuliwa na mashambulio ya maumivu mara kwa mara sababu ya kukwama kwa seli hizo na kuzuia oksijeni kwenda sehemu za viungo vya mwili.
chanzo cha ugonjwa huu ni nini?
ugonjwa huu husababishwa na kubadilika kwa mfumo wa mwili wa kutengeneza vimelea vya kutengeneza damu yaani haemoglobin. haemoglobin hii husababisha seli zinazotengenezwa kua na shepu ambayo sio ya kawaida.
ugonjwa huu hurithiwa kutoka kwa wazazi wote yaani baba na mama kitaalamu tunaita carriers.. mama na baba wanaweza kua hawana dalili yeyote lakini wamebebea vimelea vya ugonjwa huo kwenye damu zao na kumzaa mtoto mgonjwa.
mgonjwa wa sickle cell akioa au akiolewa na mtu ambaye sio mgonjwa hawezi kuzaa wagonjwa ila atazaa watoto waliobeba vimelea hivyo. watoto wenye vimelea hivyo[carriers] wakioana wanaweza kuzaa mtoto mgonjwa.
mume na mke wagonjwa wakioana watazaa wagonjwa watupu hivyo ni vizuri kuliangalia hili kabla ya kuamua kuzaa.
dalili za ugonjwa huu ni zipi?
mgonjwa wa sikoseli haonyeshi dalili yeyote mpaka afikishe miezi minne ya umri tangu kuzaliwa na huanza na dalili zifuatazo.
Kuishiwa damu; kama nilivyosema mwanzoni seli za sikoseli huishi sio zaidi ya siku ishirini hivyo vifo hivi vya seli husababisha sehemu kubwa ya mwili kukosa hewa ya kutosha ya oksijeni na kusababishwa mwili kua na uchovu sana.
Maumivu makali ya mwili; kukwama kwa seli hizi ambazo shepu zake zimekaa vibaya huzuia damu nyingi kupita kwenda sehemu mbalimbali za mwili. sehemu hizo zikikosa hewa ya oksijeni na kusababisha maumivu makali sana. maumivu hayo hua ya jointi, kifua na tumbo mara nyingi.
Kuvimba vidole; hali hii pia husababisha na kukwama kwa seli hizo za mgonjwa na kusababisha ukosefu wa oksijeni ya kutosha kwenye vidole vya mikonoo hivyo vidole huvimba na kuuma sana.
Kuchelewa kukua kwa watoto; ukosefu wa hewa ya kutosha kwenye mfumo wa damu huukosesha mwili vitamini na madini ya kutosha na hali hii husababisha kuchelewa kukua na kuchelewa kubalehe au kuvunja ungo.
Kutoona vizuri: mishipa midogo ya damu ya kwenye macho huweza kuziba na kufanya uwezo wa kuona kua mdogo sana.
Vipimo vinavyofanyika kugundua ugonjwa huu.
Kipimo cha damu; kipimo kidogo cha damu huchukuliwa na kupimwa na majibu hutolewa baada ya masaa 24. vipimo hivi ni rahisi na hupatikana karibia kwenye maabara zote nchini.
Vipimo kipindi cha ujauzito; nchi zilizoendelea mtoto aliyeko tumboni huweza kugundulika kama ni mgonjwa au sio mgonjwa na mama kuamua kama anataka kuendelea na ujauzito au vipi.
Matibabu ya sikoseli;
kubadilisha kwa vitoa damu ndani ya mifupa [bone marrow transplant] huweza kutibu ugonjwa huu kabisa lakini upasuaji huu ni mgumu sana, sio rahisi kumpata mtu atakayekutolea ambaye atafanana na wewe kwenye vipimo vitakavyotakiwa, lakini pia kuna hatari kubwa ya kupata madhara makubwa hadi kifo na upasuaji huu hufanyika nchi zilizoendelea kwa gharama kubwa sana.
hivyo matibabu ya siko seli mara nyingi hulenga kupunguza makali ya ugonjwa mara nyingi ili kumfanya mgonjwa aishi maisha ya kawaida.. dawa ambazo hutolewa ni kama zifuatazo.
Folic acid; hivi ni virutubisho ambavyo hutolewa kuongeza damu kwa mgonjwa huu na dose hua ni kidonge kimoja yaani 5mg kila siku kwa maisha yake yote. hii kidogo ni virutubisho vya zamani kidogo na hutolewa sana kwani serikali hujaribu kubana matumizi.
B12 PLUS and FOLIC ACID; hivi virutubisho vingine ambavyo ni bora kuliko folic acid peke yake kwani huachanganywa ni vitamini zingine ambazo pia ni maalumu kwa ajili kuongeza damu. hii hapa ina folic acid na vitamin b12, imechanganywa pia na virutubisho vya aloe vela na watumiaji wa hii mara nyingi hua na damu nyingi na hua mashambulio machache ya ugonjwa huu[crisis] kwa mwaka.ni moja ya virutubisho vya kisasa sana.nb unatakiwa uchague moja kati ya hizi, huwezi kutumia zote.
Dawa ya korokwini; dawa hii humezwa kila wiki na mgonjwa wa sikoseli kuzuia ugonjwa wa malaria. dozi hutegemea na uzito wa mgonjwa.
Matibabu mengine; mgonjwa huyu huonyesha dalili hizo akipata ugonjwa mwingine kama malaria, UTI, na mengine mengi hivyo mgonjwa hutibiwa kama watu wengine akiwa na shida hizo japokua hushambuliwa mara kwa mara kuliko watu wengine. mara nyini mgonjwa huongezewa maji haraka akifikishwa hospitali ili kufanya seli hizi zipite kirahisi.
jinsi ya kuzuia mashambulio ya mara kwa mara kwa mgonjwa;
Kunywa maji mengi: angalau glass nane kwa watu wazima kwani ukosefu wa maji mwilini huchangia kupata mashambulio ya maumivu mara kwa mara kwa wagonjwa.
Epuka joto kali au baridi kali; hali hizo mbili huweza kubadilisha PH[ kiwango cha tindikali na nyongo} kupanda sana au kushuka sana na kusababisha shambulio la maumivu.
Fanya mazoezi mara kwa mara: mazoezi huongeza mzunguko mzuri wa damu mwilini hivyo kufanya kinga ya mwili iwe vizuri.
Usitumie dawa bila kuandikiwa na daktari; baadhi ya dawa zinazotumika kwenye maduka ya madawa kama ephedrine za mafua huweza kusababisha mishipa ya damu kubana sana[vasoconstriction] na kusababishwa kukwama kwa seli za mgonjwa ndani ya mishipa ya damu.
Epuka kupanda ndege inayoruka angani sana; kadri unavyozidi kupanda juu ndivyo hewa ya oksijeni inazidi kua kidogo hivyo unaweza kupata shambulio kwenye ndege.
madhara ya ugonjwa huu kama usipofuatilia matibabu vizuri;
Upofu; mishipa ya damu inayosambaza damu kwenye macho huweza kuzibwa na seli hizo na kuharibu baadhi ya sehemu za macho na kuleta upofu kabisa.
Kuharibika kwa viungo vya mwili: ukosaji wa damu kwenye viungo kama bandama, figo na maini huweza kusababisha kushindwa kazi ka viungo hivyo na kupelekea kifo.
Kiharusi; kuziba kwa seli ndani ya mishipa ya damu ya kichwa huzababisha kupooza kwa upande mzima wa mwili kitaalamu kama kiharusi.
Pressure ya ndani ya mapafu: hii hutokea mara nyingi kwa wagonjwa watu wazima huonyesha kwa dalili ya kushindwa kupumua, na kuishiwa nguvu. mara nyingi huua haraka.[pulmonary hypertension]
Vidonda; baadhi ya sehemu za mwili kukosa damu huchangia kutokea kwa vidonda kitaalamu kama ulcer.
Mwisho; hakuna mganga wa kienyeji anaweza kukutibu huu ugonjwa ukapona kabisa, usipoteze pesa zako huko kabisa... kama kuna mtu anadai anayo dawa basi ajitangaze apewe tuzo ya dunia.fuatilia masharti ya madaktari na utaishi maisha ya kawaida kama wengine.
No comments:
Post a Comment