on
March 17, 2016March 15 2016, Rais John Pombe Magufuli aliwaapisha Wakuu wa Mikoa wapya huku akitoa siku 15 kwa Wakuu wa Mikoa wawe wamesimamia na kuondoa watumishi hewa na pia kuwakamata vijana wote ambao hawataki kufanya kazi kwa kuwapeleka katika kambi maalum ili wakalime.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene march 16 2016 amekutana na Wakuu hao wa Mikoa na kuwapa mikakati na miongozo ya kiutendaji katika majukumu yao mapya hasa katika kuchukua hatua kwa watendaji wazembe mikoani.
No comments:
Post a Comment