Thursday, March 17, 2016

Ally kiba amtaja msanii wa hip hop anaye mkubali zaidi

abla ya kuanza kufanya muziki wa kuimba, Alikiba alikuwa rapper mzuri.

Kwenye kipindi cha Chill na Sky, Kiba alinieleza kuwa alipokuwa shuleni alikuwa maarufu kutokana na uwezo wake wa kurap nyimbo za wasanii wa enzi hizo kama Profesa Jay na wengine.

Na sasa muimbaji huyo wa Lupela amemtaja msanii wa hip hop anayemkubali zaidi duniani. Naye si mwingine ni Juma Nature.

Alikiba alikuwa akijibu swali la shabiki kwenye #BaseTwitterView ya MTV Base East. Maswali mengine aliyoulizwa ni pamoja na ana uwezo wa kuimba lugha ngapi naye kujibu anaweza kuimba zote lakini kuandika ni mbili.
Share: Facebook Twitter Google+

No comments:

Post a Comment