Friday, March 25, 2016

UGANDA YARIDHIKA BOMBA KUISHIA TANGA

Waziri wa Nishati na Madini wa Uganda, Irene Muloni amesema ameridhishwa na eneo lililotengwa kwa ajili ya utekelezaji mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Ziwa Albert hadi Bandari ya Tanga.

Alitoa kauli hiyo jana alipoongoza ujumbe wa wataalamu na wawekezaji kutoka mashirika ya TOTAL, TULLOY na CNOOC ambayo yanatarajiwa kutekeleza ujenzi wa mradi huo; na kutembelea maeneo utakapojengwa mradi wa bomba la mafuta ghafi katika Bandari ya Tanga.

Muloni alisema baada ya kupata maelezo ya kina na kutembelea Bandari ya Tanga ameridhishwa na mazingira yaliyopo na kwamba wiki ijayo Serikali ya Uganda itatuma timu ya wataalamu watakaokagua maeneo yote yatakapopita mabomba na ujenzi wa matangi ya kuhifadhia ili kujionea hali halisi kabla ya kuruhusu mradi kuanza kutekelezwa.

“Nimeona taarifa ya mradi iliyowasilishwa hapa na wataalamu na pia nimepata fursa ya kutembelea Bandari ya Tanga na kimsingi nimeridhika na wiki ijayo nitatuma timu ya wataalamu ili kuja kufanya uhakiki na kushauri kabla ya utekelezaji rasmi kuanza,” alisema Muloni.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Justin Ntalikwa alisema amefurahishwa na ujio wa ujumbe huo ambao utarahisisha uamuzi wa kujengwa mradi huo nchini hasa baada Serikali ya Kenya kuanza kushawishi mradi huo ufanyike nchini humo.

“Tumethibitisha kwamba kupitia bandari hii ya Tanga tunavyo vigezo vya kuweza kutekeleza mradi huu hasa ikizingatiwa kwamba tunao mtandao mzuri wa miundombinu ya reli, barabara na bandari ambayo hata mradi utakapoanza tutaweza kuleta vifaa kwa urahisi tofauti na wenzetu wa nchini Kenya,” alisema Ntalikwa.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk James Matarajio alisema mazingira ya Bandari ya Tanga ambayo inazungukwa na visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na vingine ni salama zaidi kwa meli kufanya shughuli zake bila kukumbwa na hatari ya mawimbi makubwa ya bahari.

“Bandari ya Tanga ni tofauti kabisa na bandari nyingine ambazo zimekwisha tembelewa kama bandari ya Lamu ya nchini Kenya ambayo haifanyi kazi. Kwanza ina kina kirefu sana cha zaidi ya mita 40 wakati meli kubwa kama hizo za mafuta zinahitaji kina cha mita 18 na vile vile Bandari ya Tanga imeunganishwa na mtandao wa barabara na reli ambao unaweza kusafirisha mizigo hapa ukaipeleka Dodoma, Mwanza, Burundi hadi Uganda.

“Hivyo tunatumaini kwamba Serikali ya Uganda itakapokuwa inafanya maamuzi yake itachukua ruti ya Tanzania kama ambavyo viongozi wetu wa nchi walisaini makubaliano ya kuutekeleza huu mradi,” alisema Dk Mataragio.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela alisema mkoa huo umejipanga kupokea mradi huo na ambao utaongeza fursa za kiuchumi kwa wananchi wa Tanga na Taifa.

Mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi unatarajiwa kujengwa katika eneo lililopo kati ya visiwa vidogo vya Fungunyama, Ulenge na Chongoleani jijini Tanga na unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani bilioni nne hadi kukamilika.

Thursday, March 24, 2016

UGONJWA HATARII WA KIFAFA CHA MIMBA

Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaowapata wanawake wajawazito, hasa wenye mimba za kwanza. Kwa walio wengi, ugonjwa huu hutokana na kupanda kwa msukumo wa damu (High blood pressure). Ugonjwa huu utokeapo, mgonjwa hupatwa na degedege (convulsions).

Kifafa cha uzazi au wengine wanakiita kifafa cha mimba ni miongoni mwa matatizo
yanayosababisha vifo vya wajawazito nchini.Kifafa cha mimba kinaweza kutokea wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua au baada
ya kujifungua.

SABABU ZINAZO PELEKEA TATIZO HILO.
Sababu la tatizo bado wataalamu wa tiba duniani hawajagundua. Ila kuna baadhi sababu zinahisiwa kusababisha tatizo hili
(Predisposi ng factors). Baadhi ni pamoja na
1.Mwanamke kuwa na wenza wengi hali inayopelekea muingiliano wa Chromosomes

2.Sehemu moja ya ubongo kuwa na damu nyingi kuliko nyingine na kupelekea shinikizo la damu kuwa kubwa katika ubongo.

3 Mimba ya kwanza, hususan katika umri mdogo chini ya miaka 20 na umri mkubwa zaidi ya miaka 35.

4 Wenye mimba ya mapacha hupata zaidi kuliko mimba ya mtoto mmoja.

5 Ugonjwa wa shinikizo la damu au kisukari kabla ya kubeba mimba.

6 Kuwa na ugonjwa wa figo kwa mama mjamzito.

SABABU NYINGINE PIA NI KAMA
1.wanawake wote wenye mimba za kwanza

2.mimba za mapema kabla ya 20

3. wanawake ambao wazaz,bib au ndg zao wa karbu waliwah kupatwa na matatzo ya kifafa katka mimba zao

4. wanawake walev hasa wakiwa wajawazito

5.wavutaj wa sigara

6. wanawake wenye visukar

7.wanawake wenye presha

8.mimba za uzeeni baada ya miaka 35

9.wanawake wenye tabia ya kubadlisha badlisha wanaume

10.wanawake waliopatwa na kfafa mimba zao za kwanza kuna hatar kukpata kifafa tena mimba znazofuata

11.mimba za mapacha

12.kuzaa mara nyingi

DALILI ZA KIFAFA CHA MIMBA
1.Kuvimba na kubonyea kwa miguu(Pitting Oedema).

2.Shinikizo la damu kupanda.

3.Kuwa na protein katika mkojo.

4.Kizunguzungu na macho kuoana giza.

5.Kifafa chenyewe cha mimba.

MADHARA YA KIFAFA CHA MIMBA.
1.Mama mjamzito anaweza kupoteza maisha yeye na mtoto wake.

2.Kuzaa mtoto mfu.

3.Mama kuendelea kuwa na tatizo la kifafa maisha yako yote. (Epilepsy)

4.Mama kuendelea kuwa na tatizo la shinikizo la damu la kupanda.(High blood pressure)

5.Kuzaa mtoto mwenye uzito
pungufu.

SULUHISHO
1.Kujifungulia katika kituo cha afya.

2.Kuhudhuria Klinik wakati wa ujauzito.

3.Kumuona daktari unapokuwa na viashiria vya hatari wakati wa ujauzito kama kuvimba miguu au shinikizo la damu kupanda

Maji ya mvua ni salama kwa kunywa?

Katika maeneo yenye uhaba wa maji ya bomba, mvua ni chanzo muhimu sana cha maji ya kunywa katika ngazi ya kaya. Hivi karibuni msomaji wetu mmoja aliuliza; “Je, kuna tatizo lolote wanapata watu wanaotumia maji ya mvua kwa ajili ya kunywa?”

Kwa asili yake maji ya mvua kabla hayajafika katika anga letu huwa ni safi na salama kwa kunywa. Hata hivyo, maji hayo lazima yapite katika anga na ndipo yafike ardhini kama mvua.

Hapo ndipo hatari ya maji ya mvua inapoanza na kuongezeka zaidi yanapofika katika paa la nyumba au sehemu maalumu iliyojengwa kuvuna maji hayo na hatimaye kuhifadhiwa katika ndoo au tenki.

Maji ya mvua yanapopita katika anga hubeba vumbi, moshi na gesi mbalimbali zikiwamo carbon dioxide, oxygen, nitrogen dioxide na sulfur dioxide. Vitu hivyo hupunguza usafi na usalama wa maji ya mvua.

Uchafuzi zaidi wa maji ya mvua hutokea pale yanapofika katika paa la nyumba au sehemu maalumu iliyojengwa kuyavuna.

Maji ya mvua yanapofika katika paa au sehemu inayotumika kuyakusanya mara nyingi hubeba kemikali, vumbi, mchanga, vitu vilivyooza, majani, vinyesi vya ndege na wanyama.

Maji kama hayo yanapoingia katika chombo cha kuhifadhia yanaweza kuwa mazalia mazuri ya vijidudu vinavyosababisha magonjwa ya tumbo kama vile kuhara, homa ya tumbo, kipindupindu na hata kuzalisha mbu wanaoeneza magonjwa mbalimbali mfano malaria.

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa maji ya mvua mara tu baada ya kuvunwa huwa na vijidudu vinavyosababisha magonjwa ya tumbo, vikiwamo Giardia, Cryptosporidium, E. coli, Campylobacter, Vibrio, Salmonella, Shigella na Pseudomonas.

Maji ya mvua lazima yachemshwe kabla ya kuyatumia kwa kunywa au kupiga mswaki.

Idadi kubwa ya uchafu na vijidudu hupatikana pale mvua inapoanza kunyesha.

Watu wanashauriwa waanze kukinga au kuvuna maji dakika tano baada ya mvua kuanza kunyesha ili paa la nyumba au sehemu ingine inayotumika kukusanya maji ijisafishe kwa mvua ya kwanza.

Kwa kawaida, maji ya mvua hayana kiwango hatari cha kemikali zinazodhuru afya. Hata hivyo, mara nyingine kiwango cha kemikali ya zinc na lead huwa kikubwa kutokana na kuingia kemikali hizo kutoka katika paa la nyumba, tenki la kuhifadhia maji au angani.

Watu wanaovuna maji ya mvua kwa kiasi kikubwa, wanahimizwa kupima maji yao katika maabara za maji pale wanapoyavuna na miezi kadhaa baada ya kuyahifadhi.

Maji ya mvua yana uchachu na kiwango kidogo cha madini. Kiwango kidogo cha madini katika maji ya mvua kinayafanya maji hayo kukosa ladha ukilinganisha na maji ya kisima, mto, ziwa au bomba.

Kiasi kidogo cha madini kama calcium, magnesium, iron, na fluoride ni muhimu katika maji ili kuimarisha afya. Katika baadhi ya nchi, maji ya mvua husafishwa na kuongezwa madini muhimu kiafya na kusambazwa kwa wananchi kama maji ya kunywa.

Usafi na usalama wa maji ya mvua unategemea usafi wa paa la nyumba, gata, bomba na ndoo au tenki la kuhifadhia maji.

Wiki ijayo nitaelimisha juu ya namna bora na sahihi ya kuhifadhi maji ya mvua hasa katika matenki. Hii itasaidia sana jamii ya watu wa kipato cha chini ambao hutumia gharama kubwa kwa ajili ya kununua na kutumia muda mrefu wakitafuta maji.

Wednesday, March 23, 2016

UFAHAMU UGONJWA WA PRESHA YA KUPANDA NA MATIBABU YAKE.. [HYPERTENSION]

Hypertension ni nini? Huu ni ugonjwa ambao hugunduliwa pale presha ya damu inapokua juu sana kupita kiwango chake cha kawaida.

Kawaida damu inasukumwa na moyo kwenda sehemu mbalimbali za mwili lakini nguvu inayotumika kusukuma damu hiyo kutoka moyoni kwenda sehemu zote za mwili na ile ambayo inakuwepo kwenye mishipa ya damu wakati damu inapita ndio inaitwa presha ya damu. Hivyo binadamu yeyote lazima awe na presha ya damu lakini katika kiwango kinachohitajika ambacho ni 120\80mmhg mpaka 140\90mmhg zaidi ya hapo tunaita hypertension..

WALIOKO KWENYE HATARI YA KUPATA PRESHA..
umri mkubwa: wanaume wako katika hatari ya kupata presha kwenye umri wa miaka 45 na kuendelea na wanawake miaka 65 na kuendelea.

Rangi ya ngozi: presha ya damu inasumbua sana watu weusi na huweza kuanza katika umri mdogo zaidi na madhara makubwa kama kupooza, moyo kusimama ghafla na kufa kwa figo hutokea kwa weusi kuliko weupe.

Familia; Koo zenye wagonjwa wengi kwa presha kwani ugonjwa huu hufuata koo wakati mwingine

Unene: kadri unavyozidi kunenepa ndivyo mwili moyo unataka nguvu nyingi kusukuma damu
mwilini hivyo kuongezeka kwa presha.

Kutofanya mazoezi
Kuvuta sigara: kemikali ya nikotini huharbu mishipa ya damu na kuongeza hatari ya kuugua ugonjwa wa presha.

Kula chumvi nyingi; sodium hubakiza maji mengi mwilini na kuongeza presha ya damu.

Kunywa pombe sana; kunywa zaidi ya bia mbili kwa wanaume na zaidi ya bia moja kwa wanawake ni hatari kwa moyo na hupandisha presha ya damu.

Mawazo mengi; mawazo mengi humwaga homoni inaitwa adrenaline kwenye damu ambayo huongeza presha ya damu hivyo maisha usiyachukulie serious sana matatizo ni sehemu ya maisha.

Magonjwa Fulani Fulani: magonjwa kama kisukari na magonjwa ya figo huongeza hatari ya kuugua presha ya damu.


Kuna aina mbili za presha ya kupanda..

Primary hypertension: ambayo inakumba zaidi ya 95% ya watu na chanzo chake hakifahamiki.
Secondary hypertension: ambayo inakuwepo kwa 5% ya watu na chanzo chake kinafahamika na ambavyo ni magonjwa ya figo, magonjwa ya mishipa ya damu, magonjwa ya ubongo na mishipa ya fahamu na magonjwa ya mfumo wa homoni.


dalili zake ni zipi?
Dalili za presha mara nyingi hua hazipatikani kirahisi na ugonjwa huu hauna dalili maalumu na wakati mwingine huja kulingana na chanzo cha presha hiyo kama nilivyoeleza kwenye secondary hypertension kama ifuatavyo.

Kichwa kuuma
Kutokwa damu puani.
Kupumua kwa shida.
Kuishiwa nguvu
Moyo kukimbia sana
Kutokwa jasho kwa wingi


Vipimo vinavyofanyika hospitali..
Kupima presha kwa kutumia kipimo cha presha kitaalamu kama sphygmomanometer ambacho ikiwa mgonjwa atapimwa mara tatu kwa siku tatu tofauti masaa na kukutwa presha yake iko juu ya kawaida atahesabiwa kama mgonjwa wa presha na matibabu yake yataanza haraka. hata hivyo mgonjwa anatakiwa apimwe baada ya dakika tano za kupumzika kama alikua kwenye mizunguko yake.

Vipimo vingine huchukuliwa na daktari kujaribu kujua chanzo cha ugonjwa na madhara ambayo mgonjwa anaweza kua ameshayapata kutokana na ugonjwa huo ni X ray ya moyo kuangalia ukubwa wa moyo, kuangalia wingi wa lehemu kwenye damu{cholesterol}, ultrasound za figo zote kuangalia kama kuna shida yeyote huku, kipimo cha maabara cha mkojo kuangalia kama figo zimenza kupitisha vitu visivyotakiwa kutoka kama damu na kadhalika na kupima sukari kuangalia kama mgonjwa ana kisukari kwani magonjwa haya huambatana mara nyingi..

Matibabu ya presha
Kuna aina kuu za matibabu..

Matibabu yasiyotumia dawa {non pharmacological treatment]
matibabu ya dawa [pharmacological treatment]

hebu tuanze na matibabu yasiyotumia dawa…
punguza uzito: mpaka uzito uwe sawa na urefu wako, naomba nikwambie kama wewe una presha afu ni mnene unapoteza muda kwani ugonjwa huu utakutesa sana na utalazwa mara kwa mara.

Punguza unywaji wa pombe: kunywa pombe kupita kiasi huathiri mifumo mingi ya mwili na kama una presha haitashuka bali itakutesa mpaka ikuue hivyo kama we unakunywa pombe fuata viwango vya kiafya vya kunywa pombe. Bia mbili kwa mwanaume ndani masaa 24 na bia moja kwa mwanamke ndani ya masaa 24 na kila bia moja ikinywewa kwa muda wa saa moja.

Fanya mazoezi angalau nusu saa kwa siku: hii itakusaidia kupunguza mafuta yaliyoganda nadani ya mishipa ya damu na kushusha cholesterol nyingi ambayo ni hatari kwa afya yako. Mafuta haya ndio yanafanya presha ya damu inakua juu na husababisha vifo vya ghafla kwa sababu ya kuziba mishipa inayopeleka damu kwenye moyo.{coronary arteries}

Acha kufuta sigara: sigara inaweka kemikali nyingi za nicotini kwenye mishipa ya dmu amabayo huongeza presha maradufu na hakuna kiwango cha afadhali cha kuvuta kwani kila sigara unayofuta inakupunguzia siku za kuishi.

Acha kula nyama nyekundu zote na mafuta ya wanyama; nyama hizi zina lehemu nyingi au cholesterol, huongeza unene na mafuta mengi mwilini ni hatari sio kwa wagonjwa wa presha tu hata kwa watu ambao hawaumwi presha hivyo kama unataka nyama kula nyama nyeupe yaani samaki wa aina zote na nyama ya ndege wa aina zote mfano kuku[ wa kienyeji ni bora zaidi}, bata, njiwa, kanga, mbuni na kadhalika. Wanyama wote wanaotembea kwa miguu minne usiguse nyama zao. pia tumia mafuta ya mimea kama alizeti, mawese na korie kwani mafuta ya wanyama kama siagi ni hatari kwa afya yako.

Acha au punguza ulaji wa chumvi kwa kiasi kikubwa sana: hichi ndio kitu kikubwa ambacho wengi hawakijui, kama unaumwa presha hakikisha unakula mboga zako tofauti na watu wengine zikiwa hazina chumvi kabisa au chumvi kidogo mno, chumvi ina kimelea kinaitwa sodium ambacho huvuta maji ndani ya mwili na kupandisha sana prresha hivyo kama wewe ni mgonjwa wa presha na unatumia chumvi ujue unapoteza muda. Kuna chumvi maalumu kwa ajili ya wagonjwa wa presha ambazo zina sodium kidogo ana hizo unaweza kula unavyotaka.Chumvi hizi zinapatikana mijini mikubwa Tanzania hivyo kama wewe ni mgonjwa wa presha na uko mikoani tunaweza kukuagizia popote ulipo kama ukihitaji.

Matibabu ya dawa{ pharmacological treatment}
Mgonjwa atakapobainika na ugonjwa wa presha ataanzishiwa na matibabu hospitalini kulingana na dawa ipi itafanya kazi kwake haraka, gharama za dawa, na magonjwa yaliyoambatana na ugonjwa wake wa presha.

matibabu haya huanzishwa hospitali tu na sio kwenye duka la madawa na dawa hizi hupatikana bure kabisa kwenye hospitali za serikali.

Lengo kuu la matibabu ni kuzuia matatizo yatokanayo na presha ya damu mfano wa dawa hizo ni captopril, nifedipine, propanalol, atenolol, na zingine nyingi sana.

virutubisho mbadala;
mara nyingi presha inapata watu wenye umri mkubwa, yaani zaidi ya miaka 40.uwezo wao kuchukua virutubisho kwenye chakula ilicholiwa hua unapungua na kulingana na ubize wa maisha watu hua hawali mboga za majani hata wakila hawali za kutosha hivyo kiwango cha cholestrol au rehemu hua juu sana na kuzuia presha kushuka kirahisi. virutubisho hivi husaidi mwili kushusha cholestrol mwilini na kupunguza uzito mwilini.kama ifuatavyo...

field of greens;hivi ni virutubisho ambavyo vina mboga za majani nyingi sana ambazo hupunguza kiasi cha cholestrol au lehemu mwilini, kupunguza kiasi cha sukari mwilini kwa wagonjwa wa kisukari,husaidia mzunguko wa damu na kuondoa sumu mwilini. kwa kufanya hivi presha hupungua na kua katika hali ya kawaida lakini pia husaidia kupunguza uzito.

garcinia plus;bidhaa hizi za asili zinapatikana huko bara la asia kwenye miti inaitwa garcinia cambondia na kusindikwa marekani ili zisiharibike kwa matumizi ya binadamu.
inazuia ubadilishaji wa wanga kua mafuta mwilini hivyo kupunguza unene kwa kuyachoma mafuta.
inapunguza sana hamu ya kula na kujisikikia umeshiba muda mwingi na kupunguza uzito na kitambi zaidi na watu wa maeneo haya ya asia hutumia sana mti huu ndio maana ni wembamba.

matumizi; tumia kidonge kimoja saa moja au nusu saa kabla ya kula kutwa mara tatu.hivyo kama nilivyoeleza hapo juu hii itasaidia sana kuweka presha katika hali nzuri.ONYO;virutubisho hivi havikufanyi uache dawa za hospitali kwani hufanya kazi kuzisaidia dawa zile za hospitali kwani kuna watu wanatumia vidonge vya hospitali na presha haishuki hivyo vinatumika kama chakula tu.

Elimu kwa wagonjwa:

Ukishagundulika na presha tafadhali usiharibu fedha zako kwa waganga wa kienyeji wanaodai watakuponya kabisa, ugonjwa huu ukishaupata hauponi kabisa ila unaweza kuuweka katika hali nzuri kwa kumeza dawa za na kufuata masharti ya daktari kama nilivyoelekeza hapo juu presha maisha yako yote..


Kwa matokeo mazuri presha ya damu haitakusumbua iwapo ukifuata aina zote mbili za matibabu yaani yale ya dawa na yale yasiyo ya dawa.


Mwisho wa ugonjwa wa presha.

Watu wengi wanaogunduliwa na ugonjwa huu presha zao zitaendelea kupanda kadri umri unavyozidi kua mkubwa.
Ugonjwa huu usipotibiwa na kufuata masharti uwezekano wa kufa ni mkubwa sana ndio maana jina lake lingine ni SILENT KILLER yaani unaua kimya kimya na watu wengi ambao unasikia wamefia bafuni au usingizini wameuawa na ugonjwa huu.
Ugonjwa huu unaweza usije na dalili hata moja na kuna watu wengi sana wameshakufa bila kujua kama waliugua presha hivyo ni vizuri kupima presha yako angalau mara mbili au nne kwa mwaka.


Madhara ya mwisho ya ugonjwa wa presha..

Kupooza mwili na kushindwa kutembea kitaalamu kama kiharusi au stroke.
Figo kushindwa kufanya kazi na kufa.
Moyo kushindwa kufanya kazi.
Kupofuka kabisa.
Kuharibika vibaya kwa mishipa ya damu.

Wanasayansi: Povu la chura tiba ya vidonda

Povu linalotengenezwa na vyura wadogo kwa ajili ya kulinda mayai yao linaweza kuponya majeraha ya wagonjwa walioungua, wanasema wanasayansi.

Povu gumu linaweza kukusanywa na kutumiwa katika mchakato wa matibabu kama kizuizi baina ya bandeji na ngozi iliyoungua, wanaamini, Watafiti katika Chuo kikuu cha Strathclyde wameanza majaribio ya sehemu ya povu hilo.
Wanafanya majaribio hao kwa kutumia povu kutoka kwa vyura hao wadogo kutoka kisiwa cha Tungara huko Trinidad.

Vyura hao kutoa povu la urefu wa sentimeta 5 kulinda mayai yao dhidi ya magonjwa na hali ya hewa kwa wastani wa siku tano.


Povu hilo imetengenezwa kwa aina tano za Protini, Doctor Paul Hoskissonna wenzake wanasema wameweza kuzichunguza aina nne za protini hizi na wameanza kuzichanganya na dawa zao.

Watafiti hao watawasilisha kazi yao katika katika mkutano wa mwaka wa kituo cha uratibu wa shughuli za utafiti wa viumbe hai -Microbiology Society utakaofanyika Liverpool.

DAMU KUTOKA PUANI

Kutokwa na damu puani ni hali inayotokea watu wengi hasa wakati wa utoto na uzee. Damu hii hutoa kwenye kuta za ndani za pua. Kuta hizi zimejaa mishipa ya damu iliyo membamba na kufunikwa na kiasi kidogo cha seli laini. Kwa hali hii huwa ni rahisi kupasuka pale inapoguswa au kukutana na hali ya ukavu mkali. Inapopasuka damu humwagika na kutoka puani hali inayojulikana kwa kitaalamu kama epistaxis.

Mara nyingi hali hii huisha yenyewe bila kuhitaji matibabu, ingawa mara chache inaweza kuwa ya kuhatarisha maisha kiasi cha kuhitaji matibabu ya haraka.

Damu inaweza kutoka sehemu ya mbele au nyuma ya ndani ya pua. Mara nyingi damu hutokana sehemu ya mbele ya ndani ya kuta za pua (anterior nose bleeding).

Sababu
Kutokwa damu puani ni dalili inayoweza kusababishwa na magonjwa au hali mbalimbali zifuatazo :


Kuingiza vidole puani
Kupiga chafya au kupenga mafua kwa nguvu sana
Shinikizo la damu la kupanda
Saratani ya damu
Matatizo ya damu kushindwa kuganda
Kuumia puani kwa kujigonga, au kuvunjika mfupa wa pua
Kutumia dawa za kuzuia damu kuganda kama aspirin, clopidogrel na warfarin.
Saratani ya pua
Magonjwa ya ini au figo
Maambukizi ya bakteria au virusi kwenye pua
Matumizi ya madawa ya kuvuta puani
Kukauka kwa kuta za ndani za pua


Namna Inavyotokea
Kutokwa na damu puani hutokea hasa kwa watoto wa umri wa miaka 2-10 na watu wazima wenye umri wa miaka 50-80.

Hali hii hutokea ghafla damu ikianza kutoka puani polepole. Inaweza ikatoka kwenye tundu moja la pua au yote mawili. Wakati mwingine damu inaweza kutoka baada ya kutembea kwenye jua kali au kufanya mazoezi.

Damu inaweza kutoka wakati wa usiku ukiwa umelala na ukaimeza, kisha ikaonekana kwa kutapika damu au mabonge ya damu, au kupata choo chenye damu damu au cheusi sana.

Nini cha Kufanya
Mara nyingi kutokwa damu puani huacha baada ya muda mfupi bila kuhitaji matibabu. Unapotokwa damu puani fanya yafuatayo;


Tulia, usihangaike hangaike.
Inua kichwa chako kiwe juu ya usawa wa moyo
Inamisha kichwa chako kuelekea mbele kidogo kuzuia kumeza damu
Minya sehemu laini ya pua kwa vidole vyako kwa dakika 10 mpaka 15.

Unaweza ukatumia dawa za kupuliza puani ili kusimamisha damu isitoke.

Ikiwa damu inaendelea kutoka licha ya kuibana pua kwa dakika 15 au kupulizia dawa ya kuzuia damu kutoka, unatapika damu au kama hali hii inajirudia mara kwa mara basi onana na daktari haraka iwezekanavyo.

Matibabu ya hospitali hujumuisha;
Kuziba mshipa wa damu uliopasuka kwa umeme
Kuweka pamba zenye kemikali za kuzuia damu kutoka ndani ya pua. Hizi hukandamiza mishipa ya damu na kuzuia damu kuvuja. Hukaa kwa siku 1 mpaka 3 kabla ya kuondolewa.

MAUMIVU WAKATI WA KUFANYA MAPENZI KWA WANAWAKE

Maumivu wakati wa kufanya mapenzi ni hali inayojitokeza hasa kwa wanawake. Hujulikana kwa kitaalamu kama.

dyspareunia. Maumivu haya yanaweza kutokea wakati wa kufanya mapenzi au baada ya kufanya mapenzi. Sababu kuu za maumivu haya mara nyingi ni magonjwa ya zinaa na kupungua kwa majimaji ukeni wakati wa ngono.

Maumivu Wakati Wa Kufanya Mapenzi
Unaweza kuwa unapata maumivu wakati tendo la ngono linaendelea. Mara nyingi maumivu haya huwa kwenye kuta za uke, shingo ya uzazi au chini ya kitovu. Sababu za maumivu haya ni;


Kuchubuka ukeni kutokana na maji ya uke kupungua. Inawezekana kutokana na kutoandaliwa vizuri wakati wa mapenzi au uke kutotoa majimaji ya kutosha.
Magonjwa ya zinaa kama kisonono, klamidia, vaginitis.
Maambukizi ya shingo ya uzazi (cervicitis)
Maambukizi kwenye mirija ya uzazi. Mara nyingi amumivu hutokea chini ya kitovu au kiuononi.
Maumivu Baada ya Kufanya Mapenzi

Baada ya kukutana na mwenzi wako kingono, unaweza kuanza kupata maumivu dakika chache mpaka siku kadhaa toka mlipokutana. Maumivu ya kawaida huwa ni kwenye uke kutokana na kuchubuka wakati wa kufanya mapenzi. Unaweza kuyahisi vizuri hasa pale unapojisafisha kwa maji au wakati wa kukojoa ikiwa njia ya mkojo imechubuliwa.

Maumivu ndani ya uke kabisa, kiunoni au chini ya kitovu baada ya kufanya mapenzi mara nyingi huonesha dalili za

Maambukizi ya shingo ya uzazi
Maambukizi ya mirija ya uzazi
Saratani ya shingo ya kizazi

Dalili hii inaweza kuambatana na hali ya homa, kutokwa damu ukeni baada ya ngono, kutoa uchafu ukeni, kutapika na kichefuchefu.

Matibabu
Unapopata hali hii jichunguze vizuri. Kama maumivu hayajatokana na michubuko wakati wa mapenzi, basi onana na daktari haraka iwezekanavyo. Maambukizi ya shingo ya uzazi na mirija ya uzazi (Pelvic Inflammatory Disease – PID) huchangia kwa kiasi kikubwa hali hii. Matibabu ya haraka ni muhimu ili kupunguza madhara ya magonjwa haya.

Michubuko kutokana na kufanya mapenzi hupona yenyewe polepole. Jioshe vizuri kwa maji safi. Usipake dawa zozote mpaka uambiwe na daktari wako.

NOORAH ANATAMANI KUTOA NGOMA ILA ANAHOFIA HILI

Ukiachilia mbali aliposikika kwenye Like Father Like Son Remix ya msanii Stamina ni muda mrefu umepita hajasikika Noorah, huku wengi wakijiuliza nini sababu za ukimya wa msanii huyo.
Kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio Noorah ameeleza kuwa ukimya wake ni kuhofia kutoa ngoma ambayo haitofanya vizuri, pia hapendi kukurupuka kutoa ngoma kuwepo mipango maalum kuhusu ngoma hiyo.
Noorah amesema kuna ngoma kadhaa kali aliwahi kuzitoa siku za nyuma lakini mipango ya promo haiku na kusababisha ngoma hizo kupotea kiaina jambo ambalo hataki litokee tena kwa ngoma zijazo.
Ameweka wazi kuwa zipo ngoma kibao ambazo amerekodi tayari lakini mipango ya Promo haijaridhisha kwahiyo anaona bora kukaa kimya kuliko kuzitoa hovyo zikapotea.

Tuesday, March 22, 2016

Soudy Brown kampata Nyoshi kwenye U HEARD kuhusu uhusiano wa Maji na weupe wake.

Ikiwa leo March 22, 2015 Dunia inaadhimisha siku ya maji.. SOUDY BROWN ametuleta U HEARD kupitia XXL ya Clouds FM ambapo amemtafuta mwimbaji ambaye ni kiongozi wa bendi ya FM Academia ,Nyoshi El Sadaat kuzungumzia suala hilo.

“kwa siku mimi nakunywaga kama glasi ndogo tu, kwa siku hata mara sita au mara 10 kwa sababu ya joto, na ukiwa unakunywa maji mengi sana hata ngozi yako inakuwa vizuri, nyororo, maji yanasaidia sana kwenye mwili wa binadamu”- Nyoshi

Soud Brown:Hivi Ray Kigosi wa Bongo Movie unamjua hivi ngozi yake ni unavyoiona maji au vitu vingine?

Nyoshi..’Ni kutumia maji mengi na mazoezi tu yaani ukiwa unafanya mazoezi kisha unakunywa maji mengi utaona ngozi yako inakuwa imara kabisa inanyooka inakuwa nzuri, mimi situmii makopo muda wote kwasbabau inaweza ikaharibu ngozi kwa kawaida natumia maji kuwa msafi kuoga ngozi yangu inakuwa imara kabisa na wala si makopo‘- Nyoshi

Alichoandika Dogo Janja baada ya kuona maneno ya Instagram ya Young Dee kuhusu Babu Tale na Chid Benz

Headlines za mkali wa Hip Hop, Chid Benz bado hazikwisha kwenye mitandao ambapo leo March 22, 2016 Dogo Janja alipost kile ambacho hakupendezwa baada ya kuona maneo ya instagram ya Young Dee kuhusu Babu Tale na Chid Benz.

Baada ya video kusambaza na kuanza kuchukua headlines ikiashiria Babu Tale amejitosa kumsaidia rapper huyo Young Dee aliandika haya kupitia ukurasa wake wa instagram na kusema…‘‘Challenge kwako blaza hii ni aibu sidhani Kama kuna die hard fan wa ukweli wa chidi Kama ataipenda hii Au ata Kama ni kweli una mpango wa kumsaidia kama manager bora Afrika..! Nimeiona hii nmeshtuka tale! Babu Tale umeniangusha Kwa hili.. Starting to heal but kill the best rapper mbele ya macho ya watanzania’ – Young Dee

Maneno hayo yalionekana kumkwaza Dogo Janja ambaye naye kupitia ukurasa wake wa instagram naye alipost kile alichokiandika Young Dee na kusema…’Young Mpengaji… Mtazidi Kupenga Kisa Stress Mpaka Totoro..Nawanyima Chakula Mwaka huu Mule Magodoro! Ukiona Mwenzako Ananyolewa Na Wewe Tia Maji’ – Dogo Janja

Monday, March 21, 2016

FAHAMU VYAKULA HATARI KWA AFYA YA MTOTO MCHANGA

Kuna vyakula ambavyo hutakiwi kumpa mtoto mara tu unapomuanzishia chakula ?


Ute wa mayai, karanga na jamii ya karanga, asali,Samaki wenye gamba/wasio na mifupa na matunda machachu (cirtrus ) ni “vyakula visivyofaa

kwa mtoto mchanga” Madaktari hushauri watoto wasipewe vyakula hivi adi wanapofikisha umri fulani.



Hata hivyo ni wazi kwamba Madktari wengi wa watoto huwa na mitizamo inayopingana juu ya jambo hili. Ukweli nikwamba tafiti za hivi karibuni zaonyesha kua hakuna ushahidi uliothibitika kisayansi kua Vyakula hivi havifai kwa mtoto mchabga adi afikishe umri fulani.


Je kunasababu yoyote ya msingi kuchelewa kumpa mtoto vyakula hivi ingawa tafiti zaonyesha ni vyakula salama kwa mtoto?

Mwaka 2008, AAP walitoa ripoti ya utafiti wenye kichwa hiki cha habari ,

Effects of Early Nutritional Interventions on the Development of Atopic Disease in Infants and Children: The Role of Maternal Dietary Restriction, Breastfeeding, Timing of Introduction of Complementary Foods, and Hydrolyzed Formulas.


Tafiti hii ilionyesha hakuna sababu yoyote ya kuchelewa kumpa mtoto chakula cha aina yoyote pale unapomuanzishia chakula kwani vyakula vyote ni salama na hakuna ushahidi wowote wa kisayansi unaoonyesha kwamba kuchelewa kumpa mtoto vyakula hivi humlinda na kumuepusha na uwezekano wa kupata magonjwa yenye uhusiano au asili ya aleji yaani Atopic Deseases

“Repoti hii bado huacha dukuduka hasa kwa kuzingatia ukweli kwamba vyakula kama maziwa ya ng’ombe namaziwa ya unga ya watoto ,mayai na karanga mara nyingi huwapa watoto wadogo magonjwa yenye asili ya aleji”.



Je hii humaanisha nisalama kumpa mtoto wangu wa miezi 7 “vyakula visivyofaa kwa mtoto mchanga”?


Hapana,si salama. Ingawa ni kweli kwamba si vyakula hivi vyote husababisha magonjwa yenye asili ya aleji kwa mtoto ,nikweli kwamba vyakula hivi huatarisha afya ya mtoto kwa namna nyingine .

Kumbuka unaweza muanzishia mtoto chakula kati ya miezi 4-6 na si chini ya hapo. Wataalam wa afya wanashauri kumuhusisha Daktari wa watoto katika maamuzi yako ya kumuanzisha mtoto chakula,hasa ” vyakula visivyofaa kwa mtoto mchanga”

Chati hii ya “vyakula visivyofaa kwa mtoto mchanga” ni kwaajili yakukusaidia kutambua chakula kipi huweza kuleta madhara yapi katika afya ya mtoto.Piahuonyesha umri unaoshauriwa mtoto kuanza kula chakula hicho.Kama nilivyosema apo awali,si vyakula vyote hivi husababisha magojwa yenye asili ya aleji, na si lazima vyakula hivi vilete hathari kwa kila mtoto.

Chakula
Hathari
Umri wa kuanza kula chakula hiki
Asali Huweza kusababisha food poisoning na magojwa yasababishwayo na bakteria kwani kinga za mwili (immunity) katika utumbo wa mtoto hazijakua/komaa vyakutosha kukabiliana na bacteria hao Zaidi ya umri wa mwaka 1
Maziwa ya ng’ombe (yasiotolewa cream) Hudhoofisha afya ya mtoto kwani hayana virutubisho vyote muhimu vinavyofaa kwa makuzi na afya ya mtoto. (Maziwa ya ng’ombe hayafai kua mbadala wa maziwa ya mama au maziwa rasmi ya watoto wachanga)
Protini iliyopo kwenye maziwa yasiyotolewa cream ni ngumu kwa mtoto
kumeng’enya. Zaidi ya mwaka 1
Matunda machachu (citrus)
Huwa na asidi (acid) nyingi ambayo huweza sababisha vipele na maumivu ya tumbo kwa mtoto.(ingawa hii si aleji) Ni salama endapo mtoto atakula kwa kiasi kidogo kama tunda hili limechanganywa na matunda mengine yasiokua na asidi Zaidi ya mwaka 1
Maharage na brukoli Husababisha gesi tumboni Zaidi ya mwaka mmoja
Karanga na jamii ya karanga (korosho,kungu manga) Huweza kusababisha Aleji na Magonjwa yatokanayo na aleji. Protini yake ni ngumu kwa mtoto kumeng’enya
Hupalia (kupaliwa).vyema kutumia unga wake badala ya ile iliyoburuzwa Zaidi ya miezi sita (endapo haitampa aleji) Zaidi ya Mwaka 1 au 2
Mahindi (unga) Huweza kusababisha aleji na magonjwa yatokanayo na aleji Pia si tajiri wa virutubisho Zaidi ya miezi 6
Yai Huweza kusababisha aleji na magonjwa yatokanayo na aleji. Ni salama kula kiini cha yai tu Anaweza kula vyakula vyakuoka vilivyotiwa yai zima.(keki,mikate) Zaidi ya miezi 6
Zabibu Mbegu zake hupalia (kupaliwa) . Unaweza mpa maji yake yaliyochujwa endapo umechanganya na matunda mengine (kumbuka zabibu ina asidi nyingi) Zaidi ya miaka 2 Zaidi ya miezi 6
Samaki wenyegamba/wasiokua na mifupa (Shellfish/Crustaceans) Huweza kusababisha Aleji na magonjwa yatokanayo na aleji Inashauriwa kumpa mtoto samaki wa maji baridi Baada ya miezi 6 (ikimpa aleji jaribu baada ya miaka 2)

Chati hii na Mafunzo ya makala hii si mbadala wa Daktari wala isikufanye upuuze ushauri wa Daktari

Nimeandika makala hii kwa kutafsiri makala iliyoandikwa katika jarida la Umoja wa madaktari wa watoto wa Marekani. Wamethibitisha kua makala hiyo imeandikwa na wataalam wa afya kwa kuzingatia tafiti za shirika la afya duniani..

“It has been researched and compiled from various medical authorities such as private pediatricians, the AAP, the AAFP, and the WHO.”

Mambo (5) Ya Kuyatazama Ili Kuongeza Thamani Katika Biashara.

Huenda ukawa anafanya biashara au unapenda kufanya biashara lakini yapo baadhi ya mambo ya msingi ya kuyatazama kabla au wakati wa kufanya biashara. Tupo baadhi yetu tunashindwa kufikia malengo yetu hasa katika kuwaza au tunapofanya biashara. Leo katika makala haya nitakwenda kukueleza juu ya kujijengea misingi ili kukuza na kuongeza uthamani wa biashara.

Biashara yoyote ile endapo itafanywa kwa misingi ambayo inafaa itakuwa na faida sana. Zipo baadhi ya biashara hazikui kwa sababu ya kuzifanya biashara hizo miaka yote kwa staili moja. Kama kweli unataka kukuza biashara yako ni lazima utazame ni kwa jinsi gani unaweza kubadilisha mfumo wa kiutendaji ambao utakufanya uweze kupata faida zaidi. Biashara hata kama itakuwa ndogo au kubwa kiasi gani endapo utaifanya kwa ubunifu na umakini wa hali ya juu utaongeza wateja zaidi.

Yafuatayo ndio mambo ya msingi ya kuongeza uthamani wa biashara ili kuongeza wateja zaidi;

1. ladha na fasheni.
Kimsingi kuna baadhi ya watu huwa tunafanya biashara tu bila kuangalia vitu kama vile ladha au fasheni (mitindo inayokwenda na wakati) . Huenda ukawa haujanielewa ngoja nikupe mfano, kama wewe unafanya biashara angalia wateja wako wanakula au wanakunywa kwa sababu ya kukidhi mahitaji au kwa sababu wanaridhika na kile wanachokula au kunywa. Kama wewe unafanya biashara nyingine kama vile, nguo, viatu, magari, vitu vya ujenzi vitu vingine ni lazima uangalie vitu vinavyokwenda na wakati , kwani endapo utafanya hivyo ndivyo vitavyokufanya uongeze wateja. Tukumbuke ya kuwa kadri vitu vinavyokuwa vya fasheni ndivyo wateja wanavyozidi kuwa wengi.

2. Kipato cha wateja.
Katika kutazama ni vipi unaweza kuongeza uthamani wa biashara jambo la msingi ni kujua kipato cha wateja wako. Kama eneo ambalo unaishi wateja wako wanaoishi ni watu wa kipato cha kawaida ni lazima ujue ya kuwa bidhaa na bei lazima vilingane na wateja wako mfano huwezi kwenda kuanzisha biashara ya super market kijijini. Pia tukumbuke ya kuwa kuna baadhi za bidhaa endapo bei zitakuwa chini ndio huwa zinawateja wengi zaidi, halikadhalika kama wateja wako ni watu wa kipato cha juu basi bidhaa na bei ya bidhaa zako ni lazima yakidhi mahitaji ya watu hao kwa namna moja au nyingine.

3. Uhitaji wa bidhaa.
Katika biashara ni lazima uangalie uhitaji wa bidhaa au huduma kwa wateja wako. Kanuni za kibiashara zinasema kwamba kama bidhaa zina gharama ndogo za uuzaji na uhitaji wa wateja hua mkubwa sana na kinyume chake inawezekana pia. Pia ni lazima usome soko lako kwa maana ya kuangalia wateja wako wanahitaji nini, na ujalibu kuchua mahitaji yao na kuwahudumia bidhaa hizo ili kukidhi mahitaji yao.

4. Matangazo.
Matangazo kuhusiana na jinsi ya upatikanaji na matumizi ya bidhaa au huduma husika. Ili kuwavutia wateja juu ya biashara yako ni vyema kuitangaza bidhaa yako ili kuwafanya wateja waweze kuitambua biashara ambayo unaifanya. Katika kuitambulisha bidhaa katika matangazo ni lazima uwe mbunifu ili tangazo linapomfikia mtumiaji ahisi yeye ni sahemu ya biashara hiyo kwa maana ya kwamba mtumiaji aseme bila bidhaa hawezi kuishi.

5. Hali ya hewa.
Biashara yeyote ni lazima ujue ni kipindi gani bidhaa yako itauzika zaidi. Biashara zingine ni za msimu kwa mfano kama unauza miamvuli najua utaifanya kwa nguvu zaidi kipindi cha mvua. Hivyo kwa kuwa wewe ndo unataka kuifanya biashara au umekwisha kuanza biashara ni lazima uzingatie je biashara yako itauzika zaidi msimu gani? Ukizingatia hayo, biashara yako itakuwa ni yenye faida kubwa sana.

Kama unataka kufanya biashara au unafanya biashara na unataka kupata faida kubwa ni lazima uzingatie hayo kwa namna moja ama nyingine.

AFYA YA NGOZI : Mba na madhara yake mwilini

Hali hii hutokana na uwezo wa fangasi wa aina hii kusimamisha shughuli za uzalishaji wa homoni na kemikali inayoipa ngozi rangi yake. Hii husababisha upungufu wa kemikali na hivyo mabadiliko ya rangi ya ngozi.

Upungufu huo ya rangi ya ngozi si wa kudumu, bali ngozi hurudi kwenye hali ya kawaida ya rangi yake baada ya muda mrefu kidogo tangu maradhi halisi yalipokomeshwa. Bila matibabu maradhi haya huchukua muda kupona hivyo dawa ni muhimu ili mwenye maradhi aweze kupona upesi.

Namna ya kuyatambua
Maradhi haya ni rahisi kuyagundua ila kutokana na kufanana kwake na maradhi mengine yenye dalili kama hizi uhakiki wa vimelea vinavyosababisha maradhi haya ni muhimu.

Sehemu ya ngozi kutoka kwenye eneo lenye maambukizi huchukuliwa na kupelekwa maabara ambako sehemu hii ya ngozi huwekwa kwenye darubini maalum kwa ajili ya kuangalia vimelea hivi vya fangasi.

Nini matibabu yake?
Maradhi haya huweza kutibika kirahisi, ila mara nyingi hurudia kushambulia ngozi hasa eneo ambalo liliwahi kushambuliwa kabla.

Kutokana na uwezo wake wa kurudia kuambukiza ngozi huwa inashauriwa kwa aliyewahi kupata maradhi haya kurudia kutumia dawa ya kuua vimelea vya fangasi mara kwa mara ili kuondoa uwezekano wowote wa maradhi kurudia kushambulia.

Matibabu ya maradhi haya huhusisha dawa za kupaka zinazoua vimelea hivi vya fangasi.

Dawa za kuua vimelea vya fangasi za kunywa pia hutolewa kwa ajili ya kutibu aina hii ya fangasi lakini hushauriwa zitolewe tu kama dawa za kupaka zimeshindwa kuua vimelea hivi vya fangasi.

Maradhi yanayofana nayo:
Kuna magonjwa ambayo hufanana na maradhi haya. Mfano ;

-Pumu ya ngozi

-Vitiligo

Maradhi haya tutayazungumzia kwenye makala zijazo kwenye mtiririko huu.

Matokeo baada ya matibabu
Kama nilivyoandika hapo juu maeneo ya ngozi yaliyobadilika rangi huweza kubaki hivyo hata baada ya vimelea vya fangasi kuondolewa na dawa.

Hii inamaanisha inawezekana kabisa mgonjwa akabaki na mabaka yanayotokana na vimelea hivi vya fangasi muda mrefu hata baada ya kutumia dawa ambayo imefanikiwa kuondoa vimelea hivi vya fangasi. Hali hii mara nyingi huchanganya wagonjwa na kusababisha wagonjwa kudhani kuwa maradhi bado upo hivyo kuendelea kutumia dawa au kuanza kutumia dawa baada ya muda mfupi tangu kumaliza kutumia dawa zilizofanikisha uondoaji wa vimelea.

Hali ya sehemu ya ngozi iliyoathiriwa na vimelea vya fangasi kurudisha rangi ya kawaida ya ngozi kama sehemu nyingine ambazo hazikua na madhara huchukua muda mrefu kidogo ingawa kama eneo husika lilikua na uvimbe basi uvimbe hupotea haraka.

KATIBA YA ZANZIBAR KUHUSU NAFASI YA MAKAMO WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR!

Sehemu ya Pili
Makamo wa Kwanza wa Rais na Makamo wa Pili wa Rais

Ibara ya : 39
(1) Kutakuwa na Makamo Wawili wa Rais ambao watajulikana kama Makamo wa Kwanza wa Rais na Makamo wa Pili wa Rais.

(2) Ndani ya siku saba mara baada ya kushika madaraka, Rais atateua Makamo wa Kwanza wa Rais na Makamo wa Pili wa Rais.

(3) Makamo wa Kwanza wa Rais atatakiwa awe na sifa za kumuwezesha kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na atateuliwa na Rais baada ya kushauriana na chama kilichotokea nafasi ya pili katika matokeo ya kura ya Uchaguzi wa Rais. Isipokuwa kwamba:
(i) iwapo chama kilichotokea nafasi ya pili katika matokeo ya kura ya Uchaguzi wa Rais kimepata chini ya asilimia kumi (10) ya kura zote za Uchaguzi wa Rais, au
(ii) endapo Rais atakuwa hana mpinzani, basi nafasi ya Makamo wa Kwanza wa Rais itapewa chama chochote cha upinzani kilichotokea cha pili kwa wingi wa viti vya Majimbo katika Baraza la Wawakilishi.

Matokeo ya Uchaguzi..

BREAKING NEWSSS ... MKUU WA WILAYA NA MTANGAZAJI MKONGWE SARA DUMBA AFARIKI DUNIA

MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI.SARAH DUMBA AKIWA OFISINI KWAKE.

Habari zilizotufikia hivi zinasema Mkuu wa wilaya wa Njombe na Mtangazaji mkongwe wa Radio Tanzania,Bi. Sara Dumba amefariki Dunia. Taarifa zaidi tutazidi kuwaletea..

Sunday, March 20, 2016

Cyril Kamikaze kaguswa na headlines za Mkali wa Hip Hop Chid Benz, kayaandika haya

Headlines za msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka Ilala, Rashid Makwilo aka Chid Benz zinazidi kuchukua nafasi katika mitandao mbalimbali, sasa leo March 20, 2016 mkali Cyril Kamikaze kupitia ukurasa wake wa instagram ameonekana kuguswa na kuamua kuandika.

‘Mara nyingi binadamu anapokua kwenye matatizo ndipo kila mtu ana mnyooshea kidole , kiukweli nina fahamu pressure ya kua mtu maarufu ilivyo na wakati mwingine kama hauja jipanga vizuri ni kitu kinaweza kukutesa sana kwa sababu unapo kua mwenyewe na kuwaza inaweza kukupeleka pabaya kabisa sababu ni presha nzito sana ambayo wengii hawawezi control ata wewe ambae unaishi maisha ya kawaida ukiingia huku tulipo ungeelewa kwa sasa najua ni ngumu,kuna wengine wanajatibu kujiua wengine wanarukwa na akili wakati walikua wazima ila yote ni mambo na matatizo tunayokutana nayo duniani sometimes the state of mind inakua ngumu kua controlled’ – Cyril
‘Kuna msemo unaosema kabla hujafa hujaumbika ,Ila binadamu tuwe tunajaribu kum push mtu ata kwa uzuri Chid amekuwa akijaribu kutoa nyimbo kadhaa lakini wengi hawakutoa support ya ku post cover yake kama ambavyo hizi picha za afya yake kubadilika zilivyo trend , sio kitu kizuri kuna muda wewe kama binadamu unahitaji kujua kuna kupanda na kushuka kuna magonjwa na afya njema utajiri umaskini hili linamkuta yoyote yule haijalishi kama maarufu ama sio… Wakati huu sio wakumcheka Chid Benz ni muda wakuwa karibu na kum support’ – Cyril

‘Support yako mtanzania hata kumpa moyo kumpokea kwa ku support kazi zake zinaweza mbadilisha chid huyu mnae muona leo na kua a better person ila kejeli na maneno machafu huzidisha mawazo na kumfanya awe vibaya zaidi .. Well najua kaka yangu Rashid uko strong sana,sababu mi napata nafasi ya kuongea nawewe huo mwili wala isiwe sababu ya watu kuona namna gani vipi najua unaweza vuka kwenye hii hali naamini Mungu yuko pamoja na wewe bado nafasi ipo saaana mfalme wa ilala DONT GIVE UP !! #CHIDBENZANAWEZA #HALIYACHIDBENZSIOMWISHOWAKE #SUPPORTCHIDBENZ’ – Cyril

Nay atajwa Freemason

DAR ES SALAAM: Kutokana na muda mrefu kutajwa kuwa ni mwanachama wa Freemason, staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ameibuka na kusema kuwa hajawahi kujiunga ila kama kuna mtu anajua kama kweli kuna fedha yupo tayari kuunganishwa.

Akipiga stori na paparazzi wetu, Nay alisema mara nyingi amekuwa akionyesha na kuzitumia alama za freemason kwa sababu anazipenda lakini siyo kwamba ni mwanachama wao ila kama kuna mtu mwenye ufahamu vizuri namna fedha zinavyopatikana huko, yupo tayari kuunganishwa kwani anahitaji fedha zaidi.
“Siko freemason na sijui wanapatikana wapi, nimekuwa nikitumia alama zao hata kwenye video za nyimbo zangu kwa sababu tu nazipenda sana, lakini siyo vinginevyo,” alisema Nay.

Kwa upande mwingine Nay alisema sasa ameamua kubadili staili ya maisha baada ya kupitia kwenye misukosuko mingi ikiwa ni pamoja na gari lake kuvunjwa vioo na kutishiwa maisha kwenye simu na sehemu mbalimbali anazopita.

“Namshukuru sana mama yangu kwani amekuwa akinipigia kelele kila wakati kuhusu kubadili mwenendo wa maisha yangu, kwa mara ya kwanza nimeenda kanisani baada ya kukaa kwa miaka kumi na moja bila kukanyaga kwenye jengo hilo takatifu, hivyo naomba watu wasinifikirie vibaya,” alisema Nay.

Daktari: Maini ya Penny yameharibika!

Mtangazaji wa Zouk TV, Penniel Mungilwa ‘VJ Penny’.

Dar es Salaam: Habari mbaya! Majibu ya daktari yamemkatisha tamaa Mtangazaji wa Zouk TV, Penniel Mungilwa ‘VJ Penny’ baada ya kuambiwa kuwa, kutokana na unywaji wa pombe kali kupitiliza, maini yake yameanza kuharibika na asipochukua hatua za haraka hali itazidi kuwa mbaya zaidi.

Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Penny, hivi karibuni mrembo huyo aliyewahi kuwa mwandani wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alikuwa hajisikii vizuri na mara nyingi alipokuwa akijaribu kula, alitapika na kuishiwa nguvu hivyo akaamua kwenda kupima kwenye Hospitali ya AAR jijini Dar.

Mpashaji huyo alidai kwamba baada ya Penny kuchukua vipimo vyote, ilibainika kwenye maini yake kuna tatizo na chanzo chake ni unywaji wa pombe kali.“Maskini Penny, sasa hivi hana raha kabisa tangu daktari amwambie ana matatizo kwenye ini, mara nyingi anakuwa mnyonge na mwenye wasiwasi sana,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kupokea taarifa hiyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Penny ambapo alizungumza kwa upole kuwa angeomba vitu vingine asiviweke wazi kwenye vyombo vya habari kwani ni mambo ya kidaktari zaidi.

“Kiukweli sijisikii vizuri na hata kuongea sana naona shida. Unajua vitu vya kidaktari siyo vizuri kuviweka kwenye vyombo vya habari. Kifupi sipo vizuri,” alisema Penny akionekana kutokuwa na furaha.
Share: Facebook Twitter Google+

Hotuba Ya Kwanza Ya Ole Sendeka Kama Msemaji Wa CCM

Machi 15, 2016, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akiwaapisha Wakuu wapya wa mikoa, aliagiza pamoja na mambo mengine, viongozi katika ngazi mbalimbali kuhakikisha wanasimamia nguvu kazi ya vijana katika maeneo yao ili waache kukaa kijiweni.

Agizo hilo lililenga utekelezaji wa vitendo wa matumizi bora ya rasilimali watu nchini wakiwemo vijana ambao ni nguvu kazi muhimu kwa taifa, kujengewa mazingira mazuri yatakayowawezesha kujiajiri katika shughuli za uzalishaji mali.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinampongeza kwa dhati Rais Magufuli kwa agizo lake hilo lenye lengo muhimu la kuwafanya watanzania kwa pamoja kuwajibika.

CCM inampongeza Rais Magufuli kwani kwa mara nyingine tena amedhihirisha kuwa wapiga kura walio wengi walifanya uamuzi sahihi kwa kumchagua yeye kuwa Rais wa Serikali
ya awamu ya Tano katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.

CCM kama chama anachotoka Rais Magufuli na ambacho ndicho Ilani yake inatekelezwa na serikali kwa kupindi cha 2015/2020, ina kila sababu ya kumpongeza kwa kuanza
vizuri katika uongozi wake wa miaka mitano na tunaamini kuwa katika kipindi hicho, “Tanzania Tunayoitaka” itafika mbali kimaendeleo kwenye kila ngazi.

Historia ipo wazi kuwa wakati Tanzania inapata uhuru wake mwaka 1961, Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliongoza taifa letu na kauli mbiu ya UHURU NA KAZI baadae ikabadilika kuwa Uhuru ni Kazi na sasa awamu ya Tano inaendesha shughuli zake kwa kauli mbiu ya “HapaKaziTu” ambayo kila mmoja ni shahidi kuwa hivi sasa kazi inatekelezwa kwa kasi kubwa.

Utekelezaji wa kauli mbiu ya HapaKaziTu umejidhihirisha katika kipindi kifupi cha uongozi wa Serikali hii yak awamu ya tano katika kudhibiti rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma, matumizi mabaya ya madaraka na na ukwepaji kodi, mambo ambayo matokeo yake yameshaanza kuonekana.

Matokeo hayo ni pamoja na kuongezeka kwa makusanyo ya kodi ya serikali, ambayo yameiongezea serikali uwezo wa kuwahudumia wananchi kujikwamua na umaskini kwa
ustawi wa jamii kwa ujumla.

Aidha CCM kinamuunga mkono Rais Magufuli pia kwa hatua anazozichukua yeye na serikali yake katika kurudisha nidhamu na uwajibikani katika utumishi wa umma.

Kumbukumbu zinaonyesha mpaka sasa watumishi wa umma waliochukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma mbalimbali kwenye utumishi wao, na wengine wakifikishwa kwenye vyombo vya sheria, wamefanyiwa hivyo kwa kufuata sheria na kuzingatia misingi ya utawala bora.

Hata hivyo wapo watu wachache wameamua kupotosha nia njema ya Mheshimiwa Rais na serikali yake kwa kuonesha kuwa haya yanayofanyika ni udikteta na uonevu.

Naomba ifahamike kuwa CCM iliiagiza serikali yake kwenye ilani yake ya uchaguzi ya 2015/2020 kuhakikisha inarudisha nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma kwa hiyo kinachofanywa na Rais Magufuli na serikali yake ni utekelezaji ilani ya CCM na ndiyo mahitaji na matakwa ya watanzania walio wengi.

Watanzania walio wengi wanataka kuuona utumishi wa umma wenye nidhamu na uwajibikaji hivyo tunawaomba watanzania kuwapuuza wale wote wanaotafsiri hatua hizi kuwa ni udikteta na uvunjifu wa sheria, kwani kwa matendo yao na maneno yao wanashabikia uzembe na kutowajibika kazini jambo ambalo CCM haikubaliani nalo.

CCM inawasihi wanachama wake, wapenzi, wakereketwa, mashabiki na watanzania wote kwa ujumla kuwa mstari wa mbele kumuunga mkono kwa vitendo Rais Magufuli kwa dhamira njema aliyonayo kwa taifa letu, ili hatimaye Tanzania yenye maendeleo ifanikiwe.
………………………………………………………………………

Ndugu Christopher Ole Sendeka
MSEMAJI WA CCM
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,

20/03/2016

TPDC YATOA UFAFANUZI JUU YA UGUNDUZI WA GESI ASILIA BONDE LA RUVU MKOA WA PWANI

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linapenda kutoa maelezo kuhusu taarifa iliyotolewa na gazeti la Matanzania, Toleo namba 8129 la Jumapili tarehe 20 Machi 2016 lenye kichwa cha habari “Gesi ya Ruvu shakani”.

Taarifa hiyo ilikuwa na lengo la kupinga kile kilichoelezwa na Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo kuwa ujazo wa gesi iliyogunduliwa na Kampuni ya Dodsal ya Uarabuni wenye kukadiriwa kufikia trilioni 2.17 una mashaka.

TPDC inapenda ieleweke kwamba, Kampuni ya Dodsal iligundua gesi katika kisima cha Mambambakofi-1 kwenye kitalu cha Ruvu mwezi Aprili 2015. Taarifa za ugunduzi ziliwasilishwa baada ya kufanya yafuatayo:
1. Vipimo vya kuangalia uwezekano wa gesi au mafuta kwenye mashapo ambapo kisima kilichorongwa kitaalamu iitwayo “wireline logging”. Vipimo hivyo vilionyesha uwapo wa gesi na kwa kitaalamu inaitwa “cross over”
2. Kuchukuliwa kwa vipimo vya mgandamizo kulingana na urefu wa kisima “pressure vs depth” kwenye eneo lenye mashapo lililoonyesha uwepo wa gesi
3. Aidha zilichukuliwa sampuli za gesi katika mashapo hayo ili kubaini aina ya gesi iliyopo pamoja na tafiti zingine.

Baada ya kupitia vipimo hivyo vitatu, vikaonyesha uwapo wa gesi. Kampuni ya Dodsal ikaiarifu TPDC ambayo nayo ilipitia vipimo vya logging na pressure na kujiridhisha uwepo wa gesi asilia. Sheria inaitaka TPDC kama mwenye leseni kuiarifu Serikali kuhusu kufanyika kwa ugunduzi huo. Taarifa hiyo lazima iambatane na kiasi cha awali kinachobashiri ujazo wa gesi ambao ulikuwa ni futi za ujazo bilioni 160 (0.16TCF).

Sheria hiyo pia inamruhusu mkandarasi kuendelea kufanya uchambuzi zaidi wa kina kutumia taarifa za kisima kilichochimbwa. Kwa kufanya hivyo, Dodsal wameleta taarifa ya ongezeko la ujazo wa gesi katika eneo tajwa kiasi cha futi za ujazo trilioni 2.01. Hivyo basi, kwa ujumla wake Dodsal wameleta makadiria ya ujazo wa gesi wenye ukubwa wa trilioni 2.17.

Mkandarasi atahitajika kufanya Drill Stem Test wakati atakapoleta mpango kazi wa kuhakiki ujazo wa gesi na uwezo wa mashapo kuzalisha “appraisal program”.

Mnamo Machi 2016, Serikali imetimiza matakwa ya kisheria ya kitalu cha Ruvu kuwa na “Location” na Kampuni ya Dodsal inajiandaa kuleta mpango kazi kama inavyoelekeza sheria mpya Petroleum Act 2015 kifungu namba 64 na 65.

Imetolewa na;
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
Benjamin W. Mkapa Pensions Towers, Tower “A”,
Azikiwe/Jamhuri Street
P.O. Box 2774,
Tel. +255 22 2200103/4
Dar Es Salaam, Tanzania
Website: www.tpdc-tz.com

Saturday, March 19, 2016

TAMKO LA UMOJA WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA JUU YA KUTEKWA KWA MWANDISHI WA HABARI WA SAUTI YA UJERUMANI ( DW ) SALMA SAID.

                                           Rais wa club za waandishi wa habari tanzania(utpc)

Salma Said mwandishi wa DW Zanzibar ametoweka baada ya kutekwa na watu ambao hawajafahamika jijini Dar es salaam, hali ambayo imeleta fadhaa na mshtuko kwa waandishi, jamii na familia yake hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa marejeo Zanzibar.

Ifahamike kuwa Kazi ya mwandishi wa habari ni kutoa habari juu ya kila kinachoendelea katika jamii , hivyo kama kuna dosari , dosari hiyo ni ya jamii na sio ya anayeieleza dosari .

UTPC inalaani na kupinga utekaji uliofanywa ambao sababu zake bado hazijulikani, hivyo tunaitaka serikali kuhakikisha Salma Said anatafutwa, kupatikana na anaachiwa huru mara moja kwa kuwa Serikali ndio yenye jukumu la kulinda raia wake.

Kama utekwaji wa Salma umefanywa kutokana na kazi yake ya uandishi habari tunalaani vikali hatua hiyo, vitendo hivi havipaswi kuendelea katika nchi inayoheshimu misingi haki na Demokrasia, Vitendo vya namna hii vinadumaza na kufifisha uhuru wa habari .

Tunapinga kwa nguvu zetu zote waandishi wa habari kukamatwa na vyombo vya dola au makundi ya kihalifu kwa visingizio ama vya uchochezi au maslahi ya taifa.

Waandishi tutaendelea kufanya kazi zetu bila kujali vitisho vya aina yoyote ile kutoka kwa mtu yoyote au Serikali.

Imetolewa na
DEOGRATIUS NSOKOLO
RAIS WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA -UTPC.
March 19, 2016.

Bei ya mafuta yapaa duniani

BEI ya mafuta ghafi katika soko la dunia imepanda kutoka Dola 30.77 za Marekani kwa pipa hadi kufikia Dola 40 ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu Desemba mwaka jana.

Taarifa iliyotolewa juzi na Shirika la Habari la Marekani, CNN ilionesha bei hiyo imepanda kwa asilimia 54 ikiwa ni wiki tano baada ya kushuka hadi Dola 26.05 kwa pipa.

“Soko linakuwa sana. Tunaweza kuendelea kuona hali tete,” alisema Mkurugenzi wa timu ya nishati huko Nasdaq, Tamar Essner.

Mafuta hayo yamepanda Jumatano ya wiki hii huku wazalishaji wakuu wakiongozwa na Saudi Arabia na Urusi kukubaliana kukutana Doha- Qatar mwezi ujao kujadili masuala ya mafuta.
“Sidhani kama hili limejikita katika misingi. Bado tuko juu ya usambazaji. Tuko katikati ya mchakato wa kuliweka sawa na hilo linachukua muda,” alisema Essner.

Hapa nchini mmoja wa watendaji wa ndani ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) ambaye hakutaka jina lake liandikwe kwa sasa alisema bei hiyo inaanza kutumika baada ya miezi miwili.

“Kama mafuta yakiagizwa leo (jana) basi bei hiyo itaanza kutumika Mei 18, mwaka huu kwani bei zinabadilika kila baada ya miezi miwili. Hiyo ni crude oil (mafuta ambayo hayajachakatwa),” alisema.

MTANZANIA Jumamosi lilimtafuta kwa njia ya simu Kaimu Mkurugenzi wa Waagizaji wa Mafuta ya pamoja hapa nchini, Michael Mjinja ambaye alisema utaratibu uliopo hapa nchini ni kuagiza kila mwezi na kwamba mafuta yanayoagizwa ni yale yaliyochakatwa ambayo pia bei yake inabadilika kulingana na soko hilo.

“Ikipanda kwenye soko la dunia impact yetu ni baada ya miezi miwili, hatununui mafuta ghafi tunanunua mafuta safi, bei nayo inabadilika,” alisema Mjinja.

Alitoa mfano kuwa bei ya mafuta ghafi juzi ilikuwa pipa moja ni Dola za Marekani 40.035 na bei ya jana inapatikana leo.

“Machi 16 mwaka huu mafuta ghafi ilikuwa dola za Marekani 38.705, ilipanda karibia dola 1.3, kwa upande wa mafuta ya petroli ambayo tunaagiza Metric Tani na diseli ambayo inanunuliwa kwa pipa ni dola 46.85,” alisema Mjinja.

Hivi karibuni kuliibuka sintofahamu baada ya Ewura kusema kuwa mafuta yaliyoagizwa bila ya kushindanisha zabuni ndiyo yanayosababisha bei ya soko la ndani isishuke kadiri inavyotakiwa huku Waziri George Simbachawene ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini akisema alichukua uamuzi huo kutokana na wasiwasi wa usalama wa nchi baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu.

Simbachawene ambaye hivi sasa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) akiwa katika Serikali iliyopita aliagiza kununuliwa kwa mafuta hayo kwa Sh bilioni 40 kwa matumizi ya Septemba, Oktoba na Novemba mwaka jana bila ya kushindanisha zabuni zilizokuwa mezani.

Hatua Muhimu Za Kukusaidia Kutatua Tatizo Ulilonalo

Siku zote katika maisha ya mwanadamu changamoto au matatizo ni kitu ambacho hakikwepeki. Kila mara binadamu huyu huweza kukutana na changamoto au matatizo haya kwa njia mbalimbali. Wapo ambao wanapokutana na changamoto huweza kuzikabili kirahisi na wapo ambao hukwama kabisa.

Najua na pia naamini kabisa kwa namna yoyote ile umeshawahi kukutana na matatizo katika maisha yako tena hata bila ubishi hata kidogo. Hakuna mtu ambaye hajawahi kukutana na tatizo au changamoto. Kitu cha kujiuliza ulipokutana na tatizo hilo ulifanyaje? Ulikata tamaa au ulisonga mbele?Ni kitu gani ambacho ulifanya?

Katika siku ya leo tutaangalia njia rahisi ambazo unaweza ukazitumia kukabiliana na matatizo hasa pale unapokutana nayo. Njia hizi zitakusaidia sana uweze kutambua kuwa unaweza kufanikiwa hata kama una matatizo. Na pia utaelewa kuwa na matatizo siyo mwisho wa mafanikio. Sasa twende pamoja kujifunza.

1. Amini kila tatizo lina njia ya kutokea.
Inawezekana unaona tatizo ulilonalo ni kubwa sana kiasi cha kwamba halina dawa, lakini si kweli kila kitu kina mwisho wake, ikiwa pamoja na tatizo lako hilo. Kama lilivyoanza ndivyo hivyo litakavyoisha kitu cha kuzingatia kuwa mvumilivu, ingawa maumivu kweli yapo.

2. Tuliza akili yako.
Wakati unatafuta suluhisho la tatizo lako jitahidi sana kutuliza akili yako. Mara nyingi akili huwa haifanya kazi vizuri sana kama upo kwenye msongo mkubwa wa mawazo. Hivyo ili uweze kupata majibu sahihi ya kile unachokitaka ni vyema ukaituliza akili yako ili ikupe majibu sahihi.
SOMA; Kanuni Sita (6) Muhimu Za Kushinda Tatizo Lolote Ulilonalo.

3. Acha kutafuta majibu ya kulazimisha.
Kwa vyovyote vile tatizo ulilonalo najua lina kukera na hutaki kabisa kuendelea nalo. Sasa hapa unatakiwa kuwa mwangalifu na kitu kimoja, tafuta majibu sahihi. Acha kulazimisha majibu ambayo yanaweza yasiwe msaada kwako. tumia akili yako vizuri kupata majibu ya kweli.

4. Andika kila njia unayoona inaweza kutatua tatizo lako.
Najua unaweza ukawa una majibu kichwani unayoamini yanaweza yakakusaidia. Sasa hayo majibu unayoyaamini yanaweza kutatua tatizo lako yaandike. Yafanye majibu hayo yawe wazi ikiwezekana yaweke sehemu ya wazi, ili yaumbike vizuri kichawani mwako na kukupa majibu halisi.

5. Jiamini.
Itakuwa ni kazi bure unatafuta namna ya kutatu tatizo lako wakati huo huo hujiamini. Ni vizuri ukajiamini wewe mwenyewe kwanza na ukajua un uwezo wa kulitatua taizo hilo. Bila ya kujiamini itakuawa ngumu kulitatua tataizo lako na litachukua muda mrefu.

6. Tafuta msaada.
Hilo tatizo ulilonalo sio wewe wa kwanza kulipata. Kama ni hivyo basi tafuta msaada kwa watu wengine ambao walishawahi kupitia hali kama yako. Huwezi hiyo soma vitabu vinavyoweza kukusaidia kuhusiana na tatizo lako. Vinginevyo ukibaki peke yako itakuwa ni ngumu sana kuweza kulitatua kiurahisi.

7. Fanya tahajudi (Sala)
Katika kipindi ambacho upo kwenye maatatizo ni vyema ukajijengea utaratibu wa kufanya tahajudi au sala. Hiyo itakusaidia sana kuituliza akili yako na pengine hata kukupa majibu unayotaka moja kwa moja. Sala pia au tahajudi ina nguvu kubwa sana katika akutatua tatizo ulilonalo.

Kwa kufuata hatua hizo, kwa namna moja au nyingine zitakusaidia kuweza kukabiliana na tatizo ulilonalo. Kitu cha muhimu kwako ni kuweza kuchukua hatua na kusonga mbele.
Kwenye ujasiriamali na hata biashara kwa ujumla fedha ndio damu au uhai wa biashara yako. Pamoja na kuwa na mpango mzuri, na hata ubunifu kwenye ujasiriamali bado utahitaji fedha kwa ajili ya kuzalisha au kununua bidhaa ili uweze kuuza. Na hata baada ya kuzalisha au kununua, mapato unayopata ni muhimu sana kusimamiwa vizuri kama unataka kuendelea kuwepo kwenye biashara.

Leo utapata nafasi ya kujifunza misingi mitano ya usimamizi wa fedha kwenye biashara. Misingi hiyo ni;

1. Tenga matumizi ya biashara na matumizi yako binafsi.
Moja ya kosa kubwa linalofanywa na wajasiriamali wengi ni kuchanganya matumizi binafsi na matumizi ya biashara. Ni vigumu sana kuona faida na ukuaji wa biashara kama fedha ya matumizi yako binafsi inatoka moja kwa moja kwenye fedha ya biashara. Utaona unauza sana lakini fedha huzioni. Ili uweze kuona ukuaji halisi wa biashara na ujasiriamali tenga fedha za biashara na fedha za matumizi binafsi.

2. Jilipe mshahara kutoka kwenye biashara yako.
Najua unajiuliza sasa nitaishije kama siwezi kuchanganya matumizi ya biashara na matumizi binafsi wakati biashara ndio shughuli inayoniingizia kipato cha kuendesha maisha. Ili uweze kuwa na mtengano mzuri kati ya fedha ya matumizi binafsi na matumizi ya biashara jilipe mshahara. Unaweza kuamua kujilipa mshahara kwa siku, wiki, au mwezi. Baada ya kujilipa mshahara wako usiguse tena fedha ya biashara, hili linahitaji nidhamu ya kutosha. Njia nzuri ya kujipangia mshahara ni kujilipa kamisheni, yaani unajilipa asilimia fulani ya faida unayopata kwenye biashara. Utakapohitaji kupata mshahara mkubwa zaidi utasukumwa kufanya biashara zaidi ili upate faida kubwa na baadae kamisheni kubwa.

3. Jua tofauti ya mauzo na faida.
Hiki ni kitu rahisi sana kwenye ujasiriamali ila bado wengi wanashindwa kukifuata. Mauzo ni tofauti kabisa na faida. Kwa mfano umenunua mfuko wa sukari kwa tsh elfu 40 na kuuza tsh elfu 60 umepata faida ya tsh elfu 20 si ndio? Sasa weka fedha ya kufikisha mfuko huo kwenye eneo la biashara, weka muda uliotumia kuuza mfuko huo, weka kodi ya eneo la biashara. Ukijumlisha vyote hivi unaweza kujikuta unabaki bila ya faida yoyote. Nachotaka ujifunze kwenye mfano huu ni kwamba unaweza kuona unauza fedha nyingi sana ila hupati faida kwa sababu hujapiga vizuri mahesabu yako.

4. Epuka gharama zisizo za msingi
Sio kila kitu unachoona wajasiriamali wenzako wanafanya na wewe inabidi ufanye, hasa pale kitu hicho kinapokuwa ni gharama kwenye biashara yako. Tumia fedha kwenye matumizi ya msingi na baadae utaendelea kukua kidogo kidogo. Kama ndio unafungua ofisi yako mpya kuna vitu vingi unaweza kuepuka gharama kwa kufanya manunuzi yako vizuri. Vitu kama thamani, unaweza kununua zinazokidhi mahitaji yako na kwa bei ambayo ni nzuri kwako.

5. Fanya mahesabu ya mara kwa mara kwenye biashara yako.
Hili ni tatizo la msingi na ndipo wajasiriamali wengi wanashindwa. Watu ni wavivu wa kukaa chini na kufanya mahesabu ya biashara zao. Wengine wanaamini kwa vile biashara wanasimamia wenyewe basi wanajua kila kitu hivyo hakuna haja ya kupiga hesabu moja moja kwa kila bidhaa aliyonunua na kuuza.

Hata uwe makini kiasi gani ni lazima kuna sehemu utakosea au kupitiwa. Unapofanya mahesabu mara kwa mara kwenye biashara yako inakusaidia kujua ni wapi fedha zinapotelea na kudhibiti mianya hiyo. Pia inakujuza ni vitu gani vyenye faida kubwa na vipi ambavyo vina faida ndogo.

Mafanikio kwenye ujasiriamali yanahitaji kujipanga na kujua ni kitu gani unafanya. Ni muhimu sana kuwa na usimamizi mzuri wa fedha ili uweze kufanikiwa kwenye ujasiriamali.

Ongeza pato kwa kutengeneza siagi ya karanga

Mara nyingi, ni vizuri kuwaza kuwa kila zao unalozalisha unawezaje kuliboresha na kukupatia kipato zaidi. Wakulima wa karanga walio wengi wamezoea tu kulima na kuuza karanga mara baada ya kuvuna na kuwaacha wengine wasio wakulima wakifaidika zaidi kutokana na jasho lao.

Ni vizuri kutafuta na kujifunza njia mbalimbali zinazoweza kusaidia kuboresha uzalishaji wako na pato likawa la uhakika zaidi, ambapo badala ya kuuza karanga zikiwa mbichi. Unaweza kutengeneza siagi ya karanga ukauza ikiwa bidhaa kamili.

Namna ya kutengeneza siagi ya karanga “Peanut butter”

Chambua karanga kuhakikisha zote ni nzuri.
Kaanga, menya na upepete.
Pima uzito kisha saga mpaka ziwe laini.
Andaa sukari, chumvi na mafuta ya alizeti.
Mafuta yawe 20% ya uzito wa karanga, sukari 6% na chumvi 1.7%.
Anza kuweka sukari na chumvi huku ukiongeza mafuta kidogo kidogo mpaka ichanganyike vizuri.
Bandika jikoni moto ukiwa kidogo kwa muda wa dakika kumi na tano.
Baada ya muda huo weka kwenye vifungashio na kuweka nembo tayari kwa kupeleka sokoni.

UFAHAMU UGONJWA WA SIKOSELI NA MATIBABU YAKE [ SICKLE CELL ANAEMIA ]

sickle cell ni nini?
huu ni ugonjwa wa kurithi wa kupungukiwa damu, ambapo mgonjwa hua hana damu ya kutosha kwa sababu ya seli zake za mwili sio imara kubeba hewa ya oksijeni kupeleka sehemu mbalimbali za mwili.
kwa hali ya kawaida seli za binadamu hua na umbo la kama yai na linalovutika kiasi kwamba huweza kupita kirahisi kwenye mishipa ya damu na seli hizo huishi siku 120 yaani miezi mitatu kisha hufa kupisha zingine lakini seli za mgonjwa wa sikoseli ni ngumu yaani zipo kama shepu ya mwezi, huishi siku ishirini tu, na huweza kukwama kwenye mishipa ya damu na kuzuia damu kupita na hichi ndio chanzo kikuu cha matatizo.wagonjwa hawa husumbuliwa na mashambulio ya maumivu mara kwa mara sababu ya kukwama kwa seli hizo na kuzuia oksijeni kwenda sehemu za viungo vya mwili.

chanzo cha ugonjwa huu ni nini?
ugonjwa huu husababishwa na kubadilika kwa mfumo wa mwili wa kutengeneza vimelea vya kutengeneza damu yaani haemoglobin. haemoglobin hii husababisha seli zinazotengenezwa kua na shepu ambayo sio ya kawaida.
ugonjwa huu hurithiwa kutoka kwa wazazi wote yaani baba na mama kitaalamu tunaita carriers.. mama na baba wanaweza kua hawana dalili yeyote lakini wamebebea vimelea vya ugonjwa huo kwenye damu zao na kumzaa mtoto mgonjwa.
mgonjwa wa sickle cell akioa au akiolewa na mtu ambaye sio mgonjwa hawezi kuzaa wagonjwa ila atazaa watoto waliobeba vimelea hivyo. watoto wenye vimelea hivyo[carriers] wakioana wanaweza kuzaa mtoto mgonjwa.
mume na mke wagonjwa wakioana watazaa wagonjwa watupu hivyo ni vizuri kuliangalia hili kabla ya kuamua kuzaa.

dalili za ugonjwa huu ni zipi?
mgonjwa wa sikoseli haonyeshi dalili yeyote mpaka afikishe miezi minne ya umri tangu kuzaliwa na huanza na dalili zifuatazo.
Kuishiwa damu; kama nilivyosema mwanzoni seli za sikoseli huishi sio zaidi ya siku ishirini hivyo vifo hivi vya seli husababisha sehemu kubwa ya mwili kukosa hewa ya kutosha ya oksijeni na kusababishwa mwili kua na uchovu sana.
Maumivu makali ya mwili; kukwama kwa seli hizi ambazo shepu zake zimekaa vibaya huzuia damu nyingi kupita kwenda sehemu mbalimbali za mwili. sehemu hizo zikikosa hewa ya oksijeni na kusababisha maumivu makali sana. maumivu hayo hua ya jointi, kifua na tumbo mara nyingi.
Kuvimba vidole; hali hii pia husababisha na kukwama kwa seli hizo za mgonjwa na kusababisha ukosefu wa oksijeni ya kutosha kwenye vidole vya mikonoo hivyo vidole huvimba na kuuma sana.
Kuchelewa kukua kwa watoto; ukosefu wa hewa ya kutosha kwenye mfumo wa damu huukosesha mwili vitamini na madini ya kutosha na hali hii husababisha kuchelewa kukua na kuchelewa kubalehe au kuvunja ungo.
Kutoona vizuri: mishipa midogo ya damu ya kwenye macho huweza kuziba na kufanya uwezo wa kuona kua mdogo sana.

Vipimo vinavyofanyika kugundua ugonjwa huu.
Kipimo cha damu; kipimo kidogo cha damu huchukuliwa na kupimwa na majibu hutolewa baada ya masaa 24. vipimo hivi ni rahisi na hupatikana karibia kwenye maabara zote nchini.
Vipimo kipindi cha ujauzito; nchi zilizoendelea mtoto aliyeko tumboni huweza kugundulika kama ni mgonjwa au sio mgonjwa na mama kuamua kama anataka kuendelea na ujauzito au vipi.

Matibabu ya sikoseli;
kubadilisha kwa vitoa damu ndani ya mifupa [bone marrow transplant] huweza kutibu ugonjwa huu kabisa lakini upasuaji huu ni mgumu sana, sio rahisi kumpata mtu atakayekutolea ambaye atafanana na wewe kwenye vipimo vitakavyotakiwa, lakini pia kuna hatari kubwa ya kupata madhara makubwa hadi kifo na upasuaji huu hufanyika nchi zilizoendelea kwa gharama kubwa sana.
hivyo matibabu ya siko seli mara nyingi hulenga kupunguza makali ya ugonjwa mara nyingi ili kumfanya mgonjwa aishi maisha ya kawaida.. dawa ambazo hutolewa ni kama zifuatazo.
Folic acid; hivi ni virutubisho ambavyo hutolewa kuongeza damu kwa mgonjwa huu na dose hua ni kidonge kimoja yaani 5mg kila siku kwa maisha yake yote. hii kidogo ni virutubisho vya zamani kidogo na hutolewa sana kwani serikali hujaribu kubana matumizi.
B12 PLUS and FOLIC ACID; hivi virutubisho vingine ambavyo ni bora kuliko folic acid peke yake kwani huachanganywa ni vitamini zingine ambazo pia ni maalumu kwa ajili kuongeza damu. hii hapa ina folic acid na vitamin b12, imechanganywa pia na virutubisho vya aloe vela na watumiaji wa hii mara nyingi hua na damu nyingi na hua mashambulio machache ya ugonjwa huu[crisis] kwa mwaka.ni moja ya virutubisho vya kisasa sana.nb unatakiwa uchague moja kati ya hizi, huwezi kutumia zote.

Dawa ya korokwini; dawa hii humezwa kila wiki na mgonjwa wa sikoseli kuzuia ugonjwa wa malaria. dozi hutegemea na uzito wa mgonjwa.

Matibabu mengine; mgonjwa huyu huonyesha dalili hizo akipata ugonjwa mwingine kama malaria, UTI, na mengine mengi hivyo mgonjwa hutibiwa kama watu wengine akiwa na shida hizo japokua hushambuliwa mara kwa mara kuliko watu wengine. mara nyini mgonjwa huongezewa maji haraka akifikishwa hospitali ili kufanya seli hizi zipite kirahisi.

jinsi ya kuzuia mashambulio ya mara kwa mara kwa mgonjwa;
Kunywa maji mengi: angalau glass nane kwa watu wazima kwani ukosefu wa maji mwilini huchangia kupata mashambulio ya maumivu mara kwa mara kwa wagonjwa.
Epuka joto kali au baridi kali; hali hizo mbili huweza kubadilisha PH[ kiwango cha tindikali na nyongo} kupanda sana au kushuka sana na kusababisha shambulio la maumivu.
Fanya mazoezi mara kwa mara: mazoezi huongeza mzunguko mzuri wa damu mwilini hivyo kufanya kinga ya mwili iwe vizuri.
Usitumie dawa bila kuandikiwa na daktari; baadhi ya dawa zinazotumika kwenye maduka ya madawa kama ephedrine za mafua huweza kusababisha mishipa ya damu kubana sana[vasoconstriction] na kusababishwa kukwama kwa seli za mgonjwa ndani ya mishipa ya damu.
Epuka kupanda ndege inayoruka angani sana; kadri unavyozidi kupanda juu ndivyo hewa ya oksijeni inazidi kua kidogo hivyo unaweza kupata shambulio kwenye ndege.

madhara ya ugonjwa huu kama usipofuatilia matibabu vizuri;
Upofu; mishipa ya damu inayosambaza damu kwenye macho huweza kuzibwa na seli hizo na kuharibu baadhi ya sehemu za macho na kuleta upofu kabisa.
Kuharibika kwa viungo vya mwili: ukosaji wa damu kwenye viungo kama bandama, figo na maini huweza kusababisha kushindwa kazi ka viungo hivyo na kupelekea kifo.
Kiharusi; kuziba kwa seli ndani ya mishipa ya damu ya kichwa huzababisha kupooza kwa upande mzima wa mwili kitaalamu kama kiharusi.
Pressure ya ndani ya mapafu: hii hutokea mara nyingi kwa wagonjwa watu wazima huonyesha kwa dalili ya kushindwa kupumua, na kuishiwa nguvu. mara nyingi huua haraka.[pulmonary hypertension]
Vidonda; baadhi ya sehemu za mwili kukosa damu huchangia kutokea kwa vidonda kitaalamu kama ulcer.
Mwisho; hakuna mganga wa kienyeji anaweza kukutibu huu ugonjwa ukapona kabisa, usipoteze pesa zako huko kabisa... kama kuna mtu anadai anayo dawa basi ajitangaze apewe tuzo ya dunia.fuatilia masharti ya madaktari na utaishi maisha ya kawaida kama wengine.

Friday, March 18, 2016

MKONGO AZUA GUMZO JINSI ANAVYOWACHANGANYA MASTAA WA BONGO

KUNA mshkaji anaitwa Mwami Radjabu, wadau wanamtaja kama kijana mwenye uraia wa nchi jirani ya Kongo (DRC), kwamba ni mfanyabiashara mwenye ukwasi wa kutosha. Kutokana na mkwanja wa kutosha alionao, ana ukaribu na akina dada wengi wa Kibongo, hasa hawa wenye majina katika tasnia ya filamu, wenyewe tukiwajua zaidi kama Bongo Muvi.

Leo utasikia akitajwa kama Mkongo wa Wolper au wa Masogange, kesho yake watasema ameporwa na Hamisa Mabeto, mara utasikia sasa anajirusha na Husna Maulid na ghafla watasema hivi sasa anatesa na Wema Sepetu.

Na hawa madada wote wanaotajwa, ni mastaa wetu wanaofanya vizuri katika filamu na uanamitindo. Wamecheza sinema nyingi na kwa hakika, wanao mashabiki wa kutosha kote nchini. Kuna msemo unaosema, katika msafara wa mamba na kenge wamo. Usitegemee kuwakuta mastaa wa fani fulani katika kijiwe cha peke yao.

Kilakiwanja, wanakuwepo wote, Bongo Fleva, filamu, dansi, mitindo, soka na aina nyingine zote za michezo na burudani. Kwa maana hiyo, wakati msichana mmoja anapokuwa katika ukumbi f’lani wa burudani na mtu wake, mastaa wenzake nao wanakuwepo maeneo hayo, wakifanya yao.
inakuwa rahisi kwa mfano, mwanaume asiyejulikana anayetembea na staa, kuwafahamu mastaa wengine, kama ambavyo mastaa nao wanavyoweza kumjua ‘shemeji’ yao asiye maarufu. Hiyo inamaanisha kesho akiibuka katika ‘kiwanja’ kingine cha starehe, hata kama hakuwa na mtu wake wa jana, ataweza kukutana na shemeji zake na kuendelea na makamuzi kama kawa.

Ni hapo ndipo tabu inapotokea. Labda ni kinywaji, labda ni ofa za maisha mazuri, labda ni mapenzi, lakini kinachotokea kinakera kukisikia, kwamba mwishowa mchezo, akina dada hawa wanageukana na kujikuta wote wakiunga ‘cheni’ kwa mtu mmoja. Lakini kinachosikitisha zaidi ni kusutana kunakotokea baada ya mambo yao kufahamika.

Ooh huyu ananichukulia bwana’angu, ananifuatafuata au anikome na kadhalika. Hili siyo jambo linalopendeza kulisikia kutoka kwa watu ambao jamii inawachukulia kama kioo.

Katika zamam hizi, hivi kweli watu bado wanachukuliana mabwana? Licha ya magonjwa, lakini pia haifurahishi kuona watu tunaoamini kuwa mastaa wakipanga foleni kwa mtu, eti tu kwa sababu ana pesa.

Hii inaonesha huenda hawana njia nyingine ya kujipatia kipato zaidi ya kutegemea waleti za wanaume. Kama hivi ndivyo, niwashauri dada zangu kuachana na staili hiyo ya maisha, kwa sababu licha ya kujidhalilisha wao wenyewe, lakini pia inaleta picha mbaya kwa mashabiki na wadau wengine wanaoweza kuwazuia watoto wao kujiingiza katika fani za umaarufu, wakihofia na wao wataishi kwa kutegemea wanaume! Dada zangu kuweni makini na Mwami aliyeamua kuwadilisha kama nguo.

NI HATARII NA HURUMA...HIVI NDIVYO CHIDY BENZI ALIVYO KWA SASA

 NI HATARII NA HURUMA...HIVI NDIVYO CHIDY BENZI ALIVYO KWA SASA..

Chadema Yawafuata CCM Mahakamani

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema hakikubaliani na agizo la serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Jiji la kuwataka wanaotakiwa kuhudhuria kwenye kikao cha uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es salaam wawe ni wajumbe pekee watakaopiga kura.

Chama hicho kimekataa agizo hilo na badala yake kinataka wananchi wote wa jiji la Dar es salaam wahudhurie katika kikao hicho.

Msimamo huo wa Chadema unapingana na barua ya wito wa mkutano wa uchaguzi huo iliyoandikwa Machi 15, 2016 na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sarah Yohana, iliyosema kuwa watakaoruhusiwa kuingia katika viwanja hivyo ni wajumbe pekee ambao ni wapigakura.
Akizungumza na wanahabari jana jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Mwita Waitara alisema sheria na kanuni zinaruhusu wananchi kushiriki kikao hicho cha wazi, hivyo Yohana hana mamlaka ya kuwazuia.

“Sisi tunafuata sheria na kanuni, barua ya mkurugenzi inaeleza kinyume cha utaratibu,” alisema.

Alisema kufuatia hali hiyo, Ukawa umemwandikia barua Mkurugenzi huyo ya kutokubaliana na matakwa yake ya kuzuia wafuasi wa vyama kuingia ukumbini wakati wa uchaguzi kwani ni uvunjifu wa sheria na kwamba hawatakubali, bali watawapigania na kuhakikisha wananchi wanaingia ukumbini.

Katika hatua nyingine, Waitara alisema CCM kwa sasa inawaandaa wanachama feki wa CCM wakiongozwa na wakili Elias Nawela kufungua kesi ya madai huku wakitaka wajumbe 9 toka Zanzibar na 11 kutoka mikoa mingine kushiriki uchaguzi wa meya.

Alisema, ili kukabiliana nao, wameamua kuwafuata hukuhuko mahakamani ambapo tayari wameshatuma maombi ya kujiunga na kesi hiyo namba 39 ya mwaka 2016 huku wakiwa na mawakili wao ambapo inatarajiwa kusomwa Machi 21 mwaka huu katika Mahakama ya Kisutu.