Friday, March 25, 2016

UGANDA YARIDHIKA BOMBA KUISHIA TANGA

Waziri wa Nishati na Madini wa Uganda, Irene Muloni amesema ameridhishwa na eneo lililotengwa kwa ajili ya utekelezaji mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Ziwa Albert hadi Bandari ya Tanga.

Alitoa kauli hiyo jana alipoongoza ujumbe wa wataalamu na wawekezaji kutoka mashirika ya TOTAL, TULLOY na CNOOC ambayo yanatarajiwa kutekeleza ujenzi wa mradi huo; na kutembelea maeneo utakapojengwa mradi wa bomba la mafuta ghafi katika Bandari ya Tanga.

Muloni alisema baada ya kupata maelezo ya kina na kutembelea Bandari ya Tanga ameridhishwa na mazingira yaliyopo na kwamba wiki ijayo Serikali ya Uganda itatuma timu ya wataalamu watakaokagua maeneo yote yatakapopita mabomba na ujenzi wa matangi ya kuhifadhia ili kujionea hali halisi kabla ya kuruhusu mradi kuanza kutekelezwa.

“Nimeona taarifa ya mradi iliyowasilishwa hapa na wataalamu na pia nimepata fursa ya kutembelea Bandari ya Tanga na kimsingi nimeridhika na wiki ijayo nitatuma timu ya wataalamu ili kuja kufanya uhakiki na kushauri kabla ya utekelezaji rasmi kuanza,” alisema Muloni.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Justin Ntalikwa alisema amefurahishwa na ujio wa ujumbe huo ambao utarahisisha uamuzi wa kujengwa mradi huo nchini hasa baada Serikali ya Kenya kuanza kushawishi mradi huo ufanyike nchini humo.

“Tumethibitisha kwamba kupitia bandari hii ya Tanga tunavyo vigezo vya kuweza kutekeleza mradi huu hasa ikizingatiwa kwamba tunao mtandao mzuri wa miundombinu ya reli, barabara na bandari ambayo hata mradi utakapoanza tutaweza kuleta vifaa kwa urahisi tofauti na wenzetu wa nchini Kenya,” alisema Ntalikwa.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk James Matarajio alisema mazingira ya Bandari ya Tanga ambayo inazungukwa na visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na vingine ni salama zaidi kwa meli kufanya shughuli zake bila kukumbwa na hatari ya mawimbi makubwa ya bahari.

“Bandari ya Tanga ni tofauti kabisa na bandari nyingine ambazo zimekwisha tembelewa kama bandari ya Lamu ya nchini Kenya ambayo haifanyi kazi. Kwanza ina kina kirefu sana cha zaidi ya mita 40 wakati meli kubwa kama hizo za mafuta zinahitaji kina cha mita 18 na vile vile Bandari ya Tanga imeunganishwa na mtandao wa barabara na reli ambao unaweza kusafirisha mizigo hapa ukaipeleka Dodoma, Mwanza, Burundi hadi Uganda.

“Hivyo tunatumaini kwamba Serikali ya Uganda itakapokuwa inafanya maamuzi yake itachukua ruti ya Tanzania kama ambavyo viongozi wetu wa nchi walisaini makubaliano ya kuutekeleza huu mradi,” alisema Dk Mataragio.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela alisema mkoa huo umejipanga kupokea mradi huo na ambao utaongeza fursa za kiuchumi kwa wananchi wa Tanga na Taifa.

Mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi unatarajiwa kujengwa katika eneo lililopo kati ya visiwa vidogo vya Fungunyama, Ulenge na Chongoleani jijini Tanga na unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani bilioni nne hadi kukamilika.

Thursday, March 24, 2016

UGONJWA HATARII WA KIFAFA CHA MIMBA

Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaowapata wanawake wajawazito, hasa wenye mimba za kwanza. Kwa walio wengi, ugonjwa huu hutokana na kupanda kwa msukumo wa damu (High blood pressure). Ugonjwa huu utokeapo, mgonjwa hupatwa na degedege (convulsions).

Kifafa cha uzazi au wengine wanakiita kifafa cha mimba ni miongoni mwa matatizo
yanayosababisha vifo vya wajawazito nchini.Kifafa cha mimba kinaweza kutokea wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua au baada
ya kujifungua.

SABABU ZINAZO PELEKEA TATIZO HILO.
Sababu la tatizo bado wataalamu wa tiba duniani hawajagundua. Ila kuna baadhi sababu zinahisiwa kusababisha tatizo hili
(Predisposi ng factors). Baadhi ni pamoja na
1.Mwanamke kuwa na wenza wengi hali inayopelekea muingiliano wa Chromosomes

2.Sehemu moja ya ubongo kuwa na damu nyingi kuliko nyingine na kupelekea shinikizo la damu kuwa kubwa katika ubongo.

3 Mimba ya kwanza, hususan katika umri mdogo chini ya miaka 20 na umri mkubwa zaidi ya miaka 35.

4 Wenye mimba ya mapacha hupata zaidi kuliko mimba ya mtoto mmoja.

5 Ugonjwa wa shinikizo la damu au kisukari kabla ya kubeba mimba.

6 Kuwa na ugonjwa wa figo kwa mama mjamzito.

SABABU NYINGINE PIA NI KAMA
1.wanawake wote wenye mimba za kwanza

2.mimba za mapema kabla ya 20

3. wanawake ambao wazaz,bib au ndg zao wa karbu waliwah kupatwa na matatzo ya kifafa katka mimba zao

4. wanawake walev hasa wakiwa wajawazito

5.wavutaj wa sigara

6. wanawake wenye visukar

7.wanawake wenye presha

8.mimba za uzeeni baada ya miaka 35

9.wanawake wenye tabia ya kubadlisha badlisha wanaume

10.wanawake waliopatwa na kfafa mimba zao za kwanza kuna hatar kukpata kifafa tena mimba znazofuata

11.mimba za mapacha

12.kuzaa mara nyingi

DALILI ZA KIFAFA CHA MIMBA
1.Kuvimba na kubonyea kwa miguu(Pitting Oedema).

2.Shinikizo la damu kupanda.

3.Kuwa na protein katika mkojo.

4.Kizunguzungu na macho kuoana giza.

5.Kifafa chenyewe cha mimba.

MADHARA YA KIFAFA CHA MIMBA.
1.Mama mjamzito anaweza kupoteza maisha yeye na mtoto wake.

2.Kuzaa mtoto mfu.

3.Mama kuendelea kuwa na tatizo la kifafa maisha yako yote. (Epilepsy)

4.Mama kuendelea kuwa na tatizo la shinikizo la damu la kupanda.(High blood pressure)

5.Kuzaa mtoto mwenye uzito
pungufu.

SULUHISHO
1.Kujifungulia katika kituo cha afya.

2.Kuhudhuria Klinik wakati wa ujauzito.

3.Kumuona daktari unapokuwa na viashiria vya hatari wakati wa ujauzito kama kuvimba miguu au shinikizo la damu kupanda

Maji ya mvua ni salama kwa kunywa?

Katika maeneo yenye uhaba wa maji ya bomba, mvua ni chanzo muhimu sana cha maji ya kunywa katika ngazi ya kaya. Hivi karibuni msomaji wetu mmoja aliuliza; “Je, kuna tatizo lolote wanapata watu wanaotumia maji ya mvua kwa ajili ya kunywa?”

Kwa asili yake maji ya mvua kabla hayajafika katika anga letu huwa ni safi na salama kwa kunywa. Hata hivyo, maji hayo lazima yapite katika anga na ndipo yafike ardhini kama mvua.

Hapo ndipo hatari ya maji ya mvua inapoanza na kuongezeka zaidi yanapofika katika paa la nyumba au sehemu maalumu iliyojengwa kuvuna maji hayo na hatimaye kuhifadhiwa katika ndoo au tenki.

Maji ya mvua yanapopita katika anga hubeba vumbi, moshi na gesi mbalimbali zikiwamo carbon dioxide, oxygen, nitrogen dioxide na sulfur dioxide. Vitu hivyo hupunguza usafi na usalama wa maji ya mvua.

Uchafuzi zaidi wa maji ya mvua hutokea pale yanapofika katika paa la nyumba au sehemu maalumu iliyojengwa kuyavuna.

Maji ya mvua yanapofika katika paa au sehemu inayotumika kuyakusanya mara nyingi hubeba kemikali, vumbi, mchanga, vitu vilivyooza, majani, vinyesi vya ndege na wanyama.

Maji kama hayo yanapoingia katika chombo cha kuhifadhia yanaweza kuwa mazalia mazuri ya vijidudu vinavyosababisha magonjwa ya tumbo kama vile kuhara, homa ya tumbo, kipindupindu na hata kuzalisha mbu wanaoeneza magonjwa mbalimbali mfano malaria.

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa maji ya mvua mara tu baada ya kuvunwa huwa na vijidudu vinavyosababisha magonjwa ya tumbo, vikiwamo Giardia, Cryptosporidium, E. coli, Campylobacter, Vibrio, Salmonella, Shigella na Pseudomonas.

Maji ya mvua lazima yachemshwe kabla ya kuyatumia kwa kunywa au kupiga mswaki.

Idadi kubwa ya uchafu na vijidudu hupatikana pale mvua inapoanza kunyesha.

Watu wanashauriwa waanze kukinga au kuvuna maji dakika tano baada ya mvua kuanza kunyesha ili paa la nyumba au sehemu ingine inayotumika kukusanya maji ijisafishe kwa mvua ya kwanza.

Kwa kawaida, maji ya mvua hayana kiwango hatari cha kemikali zinazodhuru afya. Hata hivyo, mara nyingine kiwango cha kemikali ya zinc na lead huwa kikubwa kutokana na kuingia kemikali hizo kutoka katika paa la nyumba, tenki la kuhifadhia maji au angani.

Watu wanaovuna maji ya mvua kwa kiasi kikubwa, wanahimizwa kupima maji yao katika maabara za maji pale wanapoyavuna na miezi kadhaa baada ya kuyahifadhi.

Maji ya mvua yana uchachu na kiwango kidogo cha madini. Kiwango kidogo cha madini katika maji ya mvua kinayafanya maji hayo kukosa ladha ukilinganisha na maji ya kisima, mto, ziwa au bomba.

Kiasi kidogo cha madini kama calcium, magnesium, iron, na fluoride ni muhimu katika maji ili kuimarisha afya. Katika baadhi ya nchi, maji ya mvua husafishwa na kuongezwa madini muhimu kiafya na kusambazwa kwa wananchi kama maji ya kunywa.

Usafi na usalama wa maji ya mvua unategemea usafi wa paa la nyumba, gata, bomba na ndoo au tenki la kuhifadhia maji.

Wiki ijayo nitaelimisha juu ya namna bora na sahihi ya kuhifadhi maji ya mvua hasa katika matenki. Hii itasaidia sana jamii ya watu wa kipato cha chini ambao hutumia gharama kubwa kwa ajili ya kununua na kutumia muda mrefu wakitafuta maji.

Wednesday, March 23, 2016

UFAHAMU UGONJWA WA PRESHA YA KUPANDA NA MATIBABU YAKE.. [HYPERTENSION]

Hypertension ni nini? Huu ni ugonjwa ambao hugunduliwa pale presha ya damu inapokua juu sana kupita kiwango chake cha kawaida.

Kawaida damu inasukumwa na moyo kwenda sehemu mbalimbali za mwili lakini nguvu inayotumika kusukuma damu hiyo kutoka moyoni kwenda sehemu zote za mwili na ile ambayo inakuwepo kwenye mishipa ya damu wakati damu inapita ndio inaitwa presha ya damu. Hivyo binadamu yeyote lazima awe na presha ya damu lakini katika kiwango kinachohitajika ambacho ni 120\80mmhg mpaka 140\90mmhg zaidi ya hapo tunaita hypertension..

WALIOKO KWENYE HATARI YA KUPATA PRESHA..
umri mkubwa: wanaume wako katika hatari ya kupata presha kwenye umri wa miaka 45 na kuendelea na wanawake miaka 65 na kuendelea.

Rangi ya ngozi: presha ya damu inasumbua sana watu weusi na huweza kuanza katika umri mdogo zaidi na madhara makubwa kama kupooza, moyo kusimama ghafla na kufa kwa figo hutokea kwa weusi kuliko weupe.

Familia; Koo zenye wagonjwa wengi kwa presha kwani ugonjwa huu hufuata koo wakati mwingine

Unene: kadri unavyozidi kunenepa ndivyo mwili moyo unataka nguvu nyingi kusukuma damu
mwilini hivyo kuongezeka kwa presha.

Kutofanya mazoezi
Kuvuta sigara: kemikali ya nikotini huharbu mishipa ya damu na kuongeza hatari ya kuugua ugonjwa wa presha.

Kula chumvi nyingi; sodium hubakiza maji mengi mwilini na kuongeza presha ya damu.

Kunywa pombe sana; kunywa zaidi ya bia mbili kwa wanaume na zaidi ya bia moja kwa wanawake ni hatari kwa moyo na hupandisha presha ya damu.

Mawazo mengi; mawazo mengi humwaga homoni inaitwa adrenaline kwenye damu ambayo huongeza presha ya damu hivyo maisha usiyachukulie serious sana matatizo ni sehemu ya maisha.

Magonjwa Fulani Fulani: magonjwa kama kisukari na magonjwa ya figo huongeza hatari ya kuugua presha ya damu.


Kuna aina mbili za presha ya kupanda..

Primary hypertension: ambayo inakumba zaidi ya 95% ya watu na chanzo chake hakifahamiki.
Secondary hypertension: ambayo inakuwepo kwa 5% ya watu na chanzo chake kinafahamika na ambavyo ni magonjwa ya figo, magonjwa ya mishipa ya damu, magonjwa ya ubongo na mishipa ya fahamu na magonjwa ya mfumo wa homoni.


dalili zake ni zipi?
Dalili za presha mara nyingi hua hazipatikani kirahisi na ugonjwa huu hauna dalili maalumu na wakati mwingine huja kulingana na chanzo cha presha hiyo kama nilivyoeleza kwenye secondary hypertension kama ifuatavyo.

Kichwa kuuma
Kutokwa damu puani.
Kupumua kwa shida.
Kuishiwa nguvu
Moyo kukimbia sana
Kutokwa jasho kwa wingi


Vipimo vinavyofanyika hospitali..
Kupima presha kwa kutumia kipimo cha presha kitaalamu kama sphygmomanometer ambacho ikiwa mgonjwa atapimwa mara tatu kwa siku tatu tofauti masaa na kukutwa presha yake iko juu ya kawaida atahesabiwa kama mgonjwa wa presha na matibabu yake yataanza haraka. hata hivyo mgonjwa anatakiwa apimwe baada ya dakika tano za kupumzika kama alikua kwenye mizunguko yake.

Vipimo vingine huchukuliwa na daktari kujaribu kujua chanzo cha ugonjwa na madhara ambayo mgonjwa anaweza kua ameshayapata kutokana na ugonjwa huo ni X ray ya moyo kuangalia ukubwa wa moyo, kuangalia wingi wa lehemu kwenye damu{cholesterol}, ultrasound za figo zote kuangalia kama kuna shida yeyote huku, kipimo cha maabara cha mkojo kuangalia kama figo zimenza kupitisha vitu visivyotakiwa kutoka kama damu na kadhalika na kupima sukari kuangalia kama mgonjwa ana kisukari kwani magonjwa haya huambatana mara nyingi..

Matibabu ya presha
Kuna aina kuu za matibabu..

Matibabu yasiyotumia dawa {non pharmacological treatment]
matibabu ya dawa [pharmacological treatment]

hebu tuanze na matibabu yasiyotumia dawa…
punguza uzito: mpaka uzito uwe sawa na urefu wako, naomba nikwambie kama wewe una presha afu ni mnene unapoteza muda kwani ugonjwa huu utakutesa sana na utalazwa mara kwa mara.

Punguza unywaji wa pombe: kunywa pombe kupita kiasi huathiri mifumo mingi ya mwili na kama una presha haitashuka bali itakutesa mpaka ikuue hivyo kama we unakunywa pombe fuata viwango vya kiafya vya kunywa pombe. Bia mbili kwa mwanaume ndani masaa 24 na bia moja kwa mwanamke ndani ya masaa 24 na kila bia moja ikinywewa kwa muda wa saa moja.

Fanya mazoezi angalau nusu saa kwa siku: hii itakusaidia kupunguza mafuta yaliyoganda nadani ya mishipa ya damu na kushusha cholesterol nyingi ambayo ni hatari kwa afya yako. Mafuta haya ndio yanafanya presha ya damu inakua juu na husababisha vifo vya ghafla kwa sababu ya kuziba mishipa inayopeleka damu kwenye moyo.{coronary arteries}

Acha kufuta sigara: sigara inaweka kemikali nyingi za nicotini kwenye mishipa ya dmu amabayo huongeza presha maradufu na hakuna kiwango cha afadhali cha kuvuta kwani kila sigara unayofuta inakupunguzia siku za kuishi.

Acha kula nyama nyekundu zote na mafuta ya wanyama; nyama hizi zina lehemu nyingi au cholesterol, huongeza unene na mafuta mengi mwilini ni hatari sio kwa wagonjwa wa presha tu hata kwa watu ambao hawaumwi presha hivyo kama unataka nyama kula nyama nyeupe yaani samaki wa aina zote na nyama ya ndege wa aina zote mfano kuku[ wa kienyeji ni bora zaidi}, bata, njiwa, kanga, mbuni na kadhalika. Wanyama wote wanaotembea kwa miguu minne usiguse nyama zao. pia tumia mafuta ya mimea kama alizeti, mawese na korie kwani mafuta ya wanyama kama siagi ni hatari kwa afya yako.

Acha au punguza ulaji wa chumvi kwa kiasi kikubwa sana: hichi ndio kitu kikubwa ambacho wengi hawakijui, kama unaumwa presha hakikisha unakula mboga zako tofauti na watu wengine zikiwa hazina chumvi kabisa au chumvi kidogo mno, chumvi ina kimelea kinaitwa sodium ambacho huvuta maji ndani ya mwili na kupandisha sana prresha hivyo kama wewe ni mgonjwa wa presha na unatumia chumvi ujue unapoteza muda. Kuna chumvi maalumu kwa ajili ya wagonjwa wa presha ambazo zina sodium kidogo ana hizo unaweza kula unavyotaka.Chumvi hizi zinapatikana mijini mikubwa Tanzania hivyo kama wewe ni mgonjwa wa presha na uko mikoani tunaweza kukuagizia popote ulipo kama ukihitaji.

Matibabu ya dawa{ pharmacological treatment}
Mgonjwa atakapobainika na ugonjwa wa presha ataanzishiwa na matibabu hospitalini kulingana na dawa ipi itafanya kazi kwake haraka, gharama za dawa, na magonjwa yaliyoambatana na ugonjwa wake wa presha.

matibabu haya huanzishwa hospitali tu na sio kwenye duka la madawa na dawa hizi hupatikana bure kabisa kwenye hospitali za serikali.

Lengo kuu la matibabu ni kuzuia matatizo yatokanayo na presha ya damu mfano wa dawa hizo ni captopril, nifedipine, propanalol, atenolol, na zingine nyingi sana.

virutubisho mbadala;
mara nyingi presha inapata watu wenye umri mkubwa, yaani zaidi ya miaka 40.uwezo wao kuchukua virutubisho kwenye chakula ilicholiwa hua unapungua na kulingana na ubize wa maisha watu hua hawali mboga za majani hata wakila hawali za kutosha hivyo kiwango cha cholestrol au rehemu hua juu sana na kuzuia presha kushuka kirahisi. virutubisho hivi husaidi mwili kushusha cholestrol mwilini na kupunguza uzito mwilini.kama ifuatavyo...

field of greens;hivi ni virutubisho ambavyo vina mboga za majani nyingi sana ambazo hupunguza kiasi cha cholestrol au lehemu mwilini, kupunguza kiasi cha sukari mwilini kwa wagonjwa wa kisukari,husaidia mzunguko wa damu na kuondoa sumu mwilini. kwa kufanya hivi presha hupungua na kua katika hali ya kawaida lakini pia husaidia kupunguza uzito.

garcinia plus;bidhaa hizi za asili zinapatikana huko bara la asia kwenye miti inaitwa garcinia cambondia na kusindikwa marekani ili zisiharibike kwa matumizi ya binadamu.
inazuia ubadilishaji wa wanga kua mafuta mwilini hivyo kupunguza unene kwa kuyachoma mafuta.
inapunguza sana hamu ya kula na kujisikikia umeshiba muda mwingi na kupunguza uzito na kitambi zaidi na watu wa maeneo haya ya asia hutumia sana mti huu ndio maana ni wembamba.

matumizi; tumia kidonge kimoja saa moja au nusu saa kabla ya kula kutwa mara tatu.hivyo kama nilivyoeleza hapo juu hii itasaidia sana kuweka presha katika hali nzuri.ONYO;virutubisho hivi havikufanyi uache dawa za hospitali kwani hufanya kazi kuzisaidia dawa zile za hospitali kwani kuna watu wanatumia vidonge vya hospitali na presha haishuki hivyo vinatumika kama chakula tu.

Elimu kwa wagonjwa:

Ukishagundulika na presha tafadhali usiharibu fedha zako kwa waganga wa kienyeji wanaodai watakuponya kabisa, ugonjwa huu ukishaupata hauponi kabisa ila unaweza kuuweka katika hali nzuri kwa kumeza dawa za na kufuata masharti ya daktari kama nilivyoelekeza hapo juu presha maisha yako yote..


Kwa matokeo mazuri presha ya damu haitakusumbua iwapo ukifuata aina zote mbili za matibabu yaani yale ya dawa na yale yasiyo ya dawa.


Mwisho wa ugonjwa wa presha.

Watu wengi wanaogunduliwa na ugonjwa huu presha zao zitaendelea kupanda kadri umri unavyozidi kua mkubwa.
Ugonjwa huu usipotibiwa na kufuata masharti uwezekano wa kufa ni mkubwa sana ndio maana jina lake lingine ni SILENT KILLER yaani unaua kimya kimya na watu wengi ambao unasikia wamefia bafuni au usingizini wameuawa na ugonjwa huu.
Ugonjwa huu unaweza usije na dalili hata moja na kuna watu wengi sana wameshakufa bila kujua kama waliugua presha hivyo ni vizuri kupima presha yako angalau mara mbili au nne kwa mwaka.


Madhara ya mwisho ya ugonjwa wa presha..

Kupooza mwili na kushindwa kutembea kitaalamu kama kiharusi au stroke.
Figo kushindwa kufanya kazi na kufa.
Moyo kushindwa kufanya kazi.
Kupofuka kabisa.
Kuharibika vibaya kwa mishipa ya damu.

Wanasayansi: Povu la chura tiba ya vidonda

Povu linalotengenezwa na vyura wadogo kwa ajili ya kulinda mayai yao linaweza kuponya majeraha ya wagonjwa walioungua, wanasema wanasayansi.

Povu gumu linaweza kukusanywa na kutumiwa katika mchakato wa matibabu kama kizuizi baina ya bandeji na ngozi iliyoungua, wanaamini, Watafiti katika Chuo kikuu cha Strathclyde wameanza majaribio ya sehemu ya povu hilo.
Wanafanya majaribio hao kwa kutumia povu kutoka kwa vyura hao wadogo kutoka kisiwa cha Tungara huko Trinidad.

Vyura hao kutoa povu la urefu wa sentimeta 5 kulinda mayai yao dhidi ya magonjwa na hali ya hewa kwa wastani wa siku tano.


Povu hilo imetengenezwa kwa aina tano za Protini, Doctor Paul Hoskissonna wenzake wanasema wameweza kuzichunguza aina nne za protini hizi na wameanza kuzichanganya na dawa zao.

Watafiti hao watawasilisha kazi yao katika katika mkutano wa mwaka wa kituo cha uratibu wa shughuli za utafiti wa viumbe hai -Microbiology Society utakaofanyika Liverpool.

DAMU KUTOKA PUANI

Kutokwa na damu puani ni hali inayotokea watu wengi hasa wakati wa utoto na uzee. Damu hii hutoa kwenye kuta za ndani za pua. Kuta hizi zimejaa mishipa ya damu iliyo membamba na kufunikwa na kiasi kidogo cha seli laini. Kwa hali hii huwa ni rahisi kupasuka pale inapoguswa au kukutana na hali ya ukavu mkali. Inapopasuka damu humwagika na kutoka puani hali inayojulikana kwa kitaalamu kama epistaxis.

Mara nyingi hali hii huisha yenyewe bila kuhitaji matibabu, ingawa mara chache inaweza kuwa ya kuhatarisha maisha kiasi cha kuhitaji matibabu ya haraka.

Damu inaweza kutoka sehemu ya mbele au nyuma ya ndani ya pua. Mara nyingi damu hutokana sehemu ya mbele ya ndani ya kuta za pua (anterior nose bleeding).

Sababu
Kutokwa damu puani ni dalili inayoweza kusababishwa na magonjwa au hali mbalimbali zifuatazo :


Kuingiza vidole puani
Kupiga chafya au kupenga mafua kwa nguvu sana
Shinikizo la damu la kupanda
Saratani ya damu
Matatizo ya damu kushindwa kuganda
Kuumia puani kwa kujigonga, au kuvunjika mfupa wa pua
Kutumia dawa za kuzuia damu kuganda kama aspirin, clopidogrel na warfarin.
Saratani ya pua
Magonjwa ya ini au figo
Maambukizi ya bakteria au virusi kwenye pua
Matumizi ya madawa ya kuvuta puani
Kukauka kwa kuta za ndani za pua


Namna Inavyotokea
Kutokwa na damu puani hutokea hasa kwa watoto wa umri wa miaka 2-10 na watu wazima wenye umri wa miaka 50-80.

Hali hii hutokea ghafla damu ikianza kutoka puani polepole. Inaweza ikatoka kwenye tundu moja la pua au yote mawili. Wakati mwingine damu inaweza kutoka baada ya kutembea kwenye jua kali au kufanya mazoezi.

Damu inaweza kutoka wakati wa usiku ukiwa umelala na ukaimeza, kisha ikaonekana kwa kutapika damu au mabonge ya damu, au kupata choo chenye damu damu au cheusi sana.

Nini cha Kufanya
Mara nyingi kutokwa damu puani huacha baada ya muda mfupi bila kuhitaji matibabu. Unapotokwa damu puani fanya yafuatayo;


Tulia, usihangaike hangaike.
Inua kichwa chako kiwe juu ya usawa wa moyo
Inamisha kichwa chako kuelekea mbele kidogo kuzuia kumeza damu
Minya sehemu laini ya pua kwa vidole vyako kwa dakika 10 mpaka 15.

Unaweza ukatumia dawa za kupuliza puani ili kusimamisha damu isitoke.

Ikiwa damu inaendelea kutoka licha ya kuibana pua kwa dakika 15 au kupulizia dawa ya kuzuia damu kutoka, unatapika damu au kama hali hii inajirudia mara kwa mara basi onana na daktari haraka iwezekanavyo.

Matibabu ya hospitali hujumuisha;
Kuziba mshipa wa damu uliopasuka kwa umeme
Kuweka pamba zenye kemikali za kuzuia damu kutoka ndani ya pua. Hizi hukandamiza mishipa ya damu na kuzuia damu kuvuja. Hukaa kwa siku 1 mpaka 3 kabla ya kuondolewa.

MAUMIVU WAKATI WA KUFANYA MAPENZI KWA WANAWAKE

Maumivu wakati wa kufanya mapenzi ni hali inayojitokeza hasa kwa wanawake. Hujulikana kwa kitaalamu kama.

dyspareunia. Maumivu haya yanaweza kutokea wakati wa kufanya mapenzi au baada ya kufanya mapenzi. Sababu kuu za maumivu haya mara nyingi ni magonjwa ya zinaa na kupungua kwa majimaji ukeni wakati wa ngono.

Maumivu Wakati Wa Kufanya Mapenzi
Unaweza kuwa unapata maumivu wakati tendo la ngono linaendelea. Mara nyingi maumivu haya huwa kwenye kuta za uke, shingo ya uzazi au chini ya kitovu. Sababu za maumivu haya ni;


Kuchubuka ukeni kutokana na maji ya uke kupungua. Inawezekana kutokana na kutoandaliwa vizuri wakati wa mapenzi au uke kutotoa majimaji ya kutosha.
Magonjwa ya zinaa kama kisonono, klamidia, vaginitis.
Maambukizi ya shingo ya uzazi (cervicitis)
Maambukizi kwenye mirija ya uzazi. Mara nyingi amumivu hutokea chini ya kitovu au kiuononi.
Maumivu Baada ya Kufanya Mapenzi

Baada ya kukutana na mwenzi wako kingono, unaweza kuanza kupata maumivu dakika chache mpaka siku kadhaa toka mlipokutana. Maumivu ya kawaida huwa ni kwenye uke kutokana na kuchubuka wakati wa kufanya mapenzi. Unaweza kuyahisi vizuri hasa pale unapojisafisha kwa maji au wakati wa kukojoa ikiwa njia ya mkojo imechubuliwa.

Maumivu ndani ya uke kabisa, kiunoni au chini ya kitovu baada ya kufanya mapenzi mara nyingi huonesha dalili za

Maambukizi ya shingo ya uzazi
Maambukizi ya mirija ya uzazi
Saratani ya shingo ya kizazi

Dalili hii inaweza kuambatana na hali ya homa, kutokwa damu ukeni baada ya ngono, kutoa uchafu ukeni, kutapika na kichefuchefu.

Matibabu
Unapopata hali hii jichunguze vizuri. Kama maumivu hayajatokana na michubuko wakati wa mapenzi, basi onana na daktari haraka iwezekanavyo. Maambukizi ya shingo ya uzazi na mirija ya uzazi (Pelvic Inflammatory Disease – PID) huchangia kwa kiasi kikubwa hali hii. Matibabu ya haraka ni muhimu ili kupunguza madhara ya magonjwa haya.

Michubuko kutokana na kufanya mapenzi hupona yenyewe polepole. Jioshe vizuri kwa maji safi. Usipake dawa zozote mpaka uambiwe na daktari wako.